loader
Najivunia ukulima, umenipa heshima

Najivunia ukulima, umenipa heshima

KILIMO kimemwezesha kujenga ghorofa ambalo ujenzi wake unaendelea.

Kimemwezesha kusaidia watu wenye uhitaji maalumu katika makundi mbalimbali, wakiwemo wajane, yatima na wenye ulemavu.

Wakati anaanza shughuli za kilimo, hakuwa na elimu wala ujuzi wowote aliosomea kuhusu kilimo.

Kabla ya kuingia kwenye kilimo, alikuwa akifanya kazi za kama Meneja katika kampuni ya Magic Kingdom jijini Dar es Salaam iliyokuwa ikimiliki migahawa ya Steers,Debonair Pizza na Wheat fiel and Coco.

Huyu si mwingine, bali ni Kareen Meela; mama wa watoto watatu aliyeamua kujitosha kwenye kilimo.

Akaamua kugawanya muda wake kwa kuishi shambani na jijini. Akajikuta ndani ya wiki, anatumia siku mbili kwenda Chalinze mkoani Pwani kusimamia shughuli za shamba na nyingine akiwa kwenye makazi yake katika eneo la Salasala, jijini Dar es Salaam.

Aliingia shambani kwa moyo wote akiwa na maono na ndoto kubwa kwamba jasho lake shambani linaweza kumtoa hatua moja na kumuweka ya juu zaidi.

Baada ya kupita milima na mabonde, Kareen anaamini sehemu kubwa ya maono na ndoto yake imetimia.

Mwanadada huyu sasa ni miongoni mwa wakulima wenye mafanikio akiwa Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa mashamba ya AKSVIN na amekuwa mlango wa msaada kwa wengine kwa kutoa ajira na kusaidia wenye uhitaji.

Baada ya kupitia changamoto kadha wa kadha, mafanikio ya kiuchumi na kijamii anayoshuhudia, yamemdhihirishia kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa maisha. “Niliazimia kutokata tamaa ingawa safari haikuwa rahisi, ” anasema.

Kareen anaeleza alivyoanza shughuli za kilimo akisema, shamba lake lipo Chalinze, mkoani Pwani.

Alinunua ekari 100 ya ardhi na alianza kulima ekari 10 kwa kilimo cha bustani. Ndani ya ekari hizo, alipanda migomba kwa kuchanganya aina mbalimbali za ndizi ikiwamo mzuzu, malindi, bukoba, mshale. Pia alipanda miti 7,000.

Kareen anasema pia alipata mbegu mseto ya miti mifupi ya mipapai na alipanda ekari mbili za pilipili (pilipili kichaa) kwa mkataba wa kulima kwa ajili ya kuuza nje. Pia alipanda miti ya matunda aina ya ‘passion’, matikiti maji, nyanya, pilipili hoho na mboga nyingine za majani.

Kwa mujibu wa Kareen, miaka minne tangu alipoanza kulima kikamilifu katika eneo la Chalinze mkoani Pwani, amefanikiwa kuajiri wafanyakazi 10 wanaokuwapo wakati wote kwa ajili ya kuangalia shamba.

Licha ya kutenga siku mbili kwa kwenda kusimamia shughuli za shamba, vile vile Kareen ameunda kundi la WhatsApp na wafanyakazi wake ambalo linamrahisishia kupokea taarifa ya kinachoendelea shambani.

Kila mfanyakazi hutoa taarifa ya anachofanya kila siku shambani. Isitoshe, ameweka utaratibu wa kuwapa zawadi wanaopata mavuno, mauzo.

Wafanyakazi wake wote wameweka nia ya kufanya kazi ikizingatiwa kwamba, amewawekea utaratibu wa kupata zawadi kubwa kwa wale wanaopata mavuno, mauzo mazuri pamoja na faida. Kareen anaeleza siri ya mafanikio katika kilimo akisisitiza umuhimu wa kufanya utafiti wa kutosha.

“Kama unataka kufanikiwa katika kilimo, unatakiwa kufanya utafiti wa kutosha na kufahamu kalenda ya mwaka mzima, ufahamu zao gani linafaa kwa msimu gani au wakatigani katika mwaka.

“Watu wengi hawafuatilii kwa undani kinachotakiwa. Unatakiwa kufahamu kila kinachohitajika katika kilimo. Mfano kiasi gani cha maji kinahitajika, joto, dawa gani ya mazao utumie, wakati gani utumie, pia unatakiwa kutafuta mbolea sahihi kwa wasambazaji wa uhakika,” anasema Kareen.

Anasema zipo mbegu nyingi katika soko na kwamba kinachotakiwa kufanyika ni kupata mbegu za uhakika kutoka kwa mtu anayetambulika. Siri nyingine ya mafanikio ni kutafuta masoko kabla ya kuvuna.

“Ili utakapofika muda wa kuvuna usipate msongo wa mawazo, wapi utapata wateja au wapi pa kupeleka bidhaa zako za shambani.Kwa kufanya hivyo inakurahisishia kudhibiti soko,” anasema.

Anatoa mfano, mwaka 2016 alikodi shamba akilenga kuanza kupanda matikiti maji. Anasema wakati huo kilimo cha matikitimaji kilikuwa kimepamba moto na kila aliyekuwa na shamba alitaka kupata matunda hayo.

Lakini alikuja kubaini kuwa soko lilikuwa limeharibika na kiwango cha mauzo kilikuwa chini kuliko gharama alizotumia kuandaa, kulima na kutunza shamba. Aliamua kusitisha na kutafuta shamba lingine sehemu nyingine.

Aliamua kununua eneo kubwa la ardhi Chalinze na kuamua kulima mihogo. Alisafisha ekari 10 na kupanda zao hilo. Alinunua mbegu kutoka Kabuku mkoani Tanga.

Hata hivyo, anasema hakuna mafanikio yasiyokuwa na mtihani au changamoto kwani alipokaribia kuvuna, nguruwe pori walivamia shamba na kula karibu kila kitu kilichokuwa shambani. Pia kilichobaki kiliibwa na watu.

Kwa mujibu wa Kareen, alikuwa amewekeza Sh milioni 1.5 kwenye shamba hilo ambalo hakuambulia chochote.

Anaeleza zaidi changamoto, alisema kwamba alipoanza hakuwa na taarifa za kutosha kuhusu kilimo hicho hivyo alijikuta akiangukia mikononi mwa wadanganyifu.

Kareen anasema baadaye alitambulishwa kwenye taasisi inayojulikana kwa kusaidia shughuli za kilimo cha bustani. Alipewa mtaalamu wa kilimo ambaye mwisho alimpatia mbegu mbaya na vifaa duni vya kilimo.

Wakati akiwa amewekeza zaidi ya Sh milioni nne kwa ajili ya miche, baada ya mavuno aliambulia Sh milioni moja. Lakini Kareen hakukata tamaa.

Alitambua kwamba anatakiwa kufanya kazi kwa bidii zaidi, kupata taarifa sahihi za kilimo na kusimama mwenyewe badala ya kuamini yeyote shambani. Kuhusu changamoto ya maji, alilazimika kuchimba kisima chenye urefu wa meta 150 kwa ajili ya kumwagilia ambacho kilimgharimu zaidi ya Sh milioni 10.

Kwa kuwa katika eneo hilo la shamba hapakuwa na umeme, ilimlazimu kuwekeza jenereta zilizogharimu Sh 4, 000, 000. Alijenga vyumba kwa ajili ya wafanyakazi.

Aliajiri meneja mzuri wa kusimamia shamba na wakati huo aliwekeza katika kilimo cha nyanya. Kareen anasema alianza kuona mwanga. Walianza kulima Oktoba na hadi kufika Januari, soko la nyanya lilikuwa juu.

Anasema kawaida Januari na Machi nyanya huwa katika uhitaji mkubwa kisha hushuka kati ya Mei na Septemba. Wakati wa mahitaji makubwa, kapu kubwa la nyanya liliuzwa Sh 110,000 kwa bei ya jumla kutoka shambani.

Wauzaji wa rejareja waliuza kilogramu kwa Sh 2,500 na kisado cha nyanya kiliuzwa Sh 17,000. “Bei hiyo ni kwa sababu ya upungufu wa nyanya uliotokea na wakulima kushindwa kuvuna nyanya za kutosha kutokana na mvua kubwamwaka jana,” anasema.

Mazao mengine anayolima ni pamoja na mahindi, mapapai, vitunguu, butternut, viazi, mchaichai, mboga za majani za aina mbalimbali na mengne mengi. Mafanikio Miongoni mwa mafanikio anayojivunia ni pamoja na kurudisha kwa jamii kwa kusaidia au kuwapa elimu na nyenzo mbalimbali.

Kareen na timu yake shambani hutoa ofa ya mafunzo kwa wakulima wadogo na kwa gharama ndogo. Anajivunia kuwa mkulima kwani amemudu kutoa ajira kwa vijana. Pia kilimo kimemkutanisha na watu wengi hasa wadau wa kilimo ndani na nje ya nchi.

Anasema kilimo pia kimemheshimisha kwani amemudu kununua gari zuri na kujikuta akipata wazo la kufungua kampuni ya kukodisha magari kwa ajili ya sherehe hususani za harusi.

“Kilimo kimeniwezesha kujenga ghorofa ambalo ujenzi wake bado unaendelea,” anaeleza zaidi kilimo kilivyomuinua kimaisha. Hata hivyo, anasema ndoto aliyo nayo ni kuvuka mipaka kwa kuuza mazao yake katika nchi mbalimbali hususani Comoro, Madagascar, Dubai, Nairobi na nchi nyingine nyingi duniani zinazotafuta mazao hususani ya bustani.mwaka jana,” anasema.

Mazao mengine anayolima ni pamoja na mahindi, mapapai, vitunguu, butternut, viazi, mchaichai, mboga za majani za aina mbalimbali na mengne mengi. Mafanikio Miongoni mwa mafanikio anayojivunia ni pamoja na kurudisha kwa jamii kwa kusaidia au kuwapa elimu na nyenzo mbalimbali.

Kareen na timu yake shambani hutoa ofa ya mafunzo kwa wakulima wadogo na kwa gharama ndogo. Anajivunia kuwa mkulima kwani amemudu kutoa ajira kwa vijana.

Pia kilimo kimemkutanisha na watu wengi hasa wadau wa kilimo ndani na nje ya nchi. Anasema kilimo pia kimemheshimisha kwani amemudu kununua gari zuri na kujikuta akipata wazo la kufungua kampuni ya kukodisha magari kwa ajili ya sherehe hususani za harusi.

“Kilimo kimeniwezesha kujenga ghorofa ambalo ujenzi wake bado unaendelea,” anaeleza zaidi kilimo kilivyomuinua kimaisha. Hata hivyo, anasema ndoto aliyo nayo ni kuvuka mipaka kwa kuuza mazao yake katika nchi mbalimbali hususani Comoro, Madagascar, Dubai, Nairobi na nchi nyingine nyingi duniani zinazotafuta mazao hususani ya bustani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/df4d6d7f35539af132caa810f9d37a10.jpg

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi