loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uwanja Taifa sasa kuitwa Uwanja wa Mkapa

RAIS John Magufuli ametangaza rasmi kwamba Uwanja wa Taifa sasa utaitwa Uwanja wa Mkapa. Rais Magufuli ameyasema hayo leo, katika hotuba yake wakati wa siku ya kitaifa ya kumuaga Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Lupaso mkoani Mtwara.

Rais Magufuli amesema mbali na Hayati Mkapa kujenga uwanja huo, amepokea maombi mengi ya watu kutaka uwanja huo uitwe kwa jina lake ingawa yeye (Mkapa) alipokuwa hai hakupenda hilo.

“Amejenga uwanja, tunaouona mbele yetu, napokea meseji nyingi wanataka uitwe uwanja wa Mkapa, nafahamu hakupenda sana vitu viitwe kwa jina lake, amelala, hawezi kuniadhibu. Natamka rasmi uwanja wa Taifa sasa utaitwa Mkapa Stadium,” amesema na kushangiliwa na umati wa watu.

“Nasikia Mkapa alikuwa shabiki mkubwa wa Yanga ingawa sikuwahi kumsikia akisema hadharani… Lakini Mzee Kikwete ananiambia hapa kwamba ni kweli,” amesema.

Kauli ya Rais Magufuli imekuja ikiwa ni siku moja baada ya mdhamini wa Simba, Mohamed Dewji kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa.

Ujenzi wa uwanja huo mkubwa kuliko vyote nchini na wenye hadhi ya Olimpiki ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ni miongoni mwa viwanja bora katika bara la Afrika kwa sasa.

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amewataka makocha wa timu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi