loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mashabiki kudhibitiwa Ligi Kuu 2020/21

VIWANJA vya michezo England huenda vikaruhusiwa kuingiza mashabiki wachache na katika msimu mpya wa Ligi Kuu 2020/21 mechi zitachezwa mbele ya mashabiki, kwa mujibu wa mshauri mkongwe wa serikali.

Serikali ya Uingereza ilitangaza mwezi huu kuruhusu baadhi ya mashabiki katika baadhi ya matukio kujaribu kutumia mwongozo mpya.

Kriketi ilikuwa mchezo wa kwanza kuhudhuriwa na mashabiki ambapo mashabiki 1,000 walitizama mechi ya kirafiki kati ya Surrey na Middlesex mwishoni mwa wiki. “Nitashangaa kama tutajaza uwanja mwaka huu,” alisema James Calder ambaye anafanya kazi na serikali kama ofisa wa afya.

“Kiukweli inahitajika kuweka muongozo na sheria kabla ya kuruhusu viwanja kuwa na mashabiki.”

Calder alisema inawezekana msimu mpya mashabiki wakaruhusiwa kuingia uwanjani lakini kwa kupunguza idadi.

“Nadhani kiuhalisia tunahitaji kuwa na tahadhari kwa siku za msimu zilizosalia lakini pia kufanya maandalizi ya msimu ujao,” aliongeza.

Calder aliongeza kuwa itafanyika kama mazoezi ya namna ya kukaa viwanjani ili kudhibiti usambaaji wa virusi vya corona.

“Kama hakutakuwa na jinsi ya udhibiti wa kusambaa kwa virusi tunaweza kufanya kwa mashabiki kukaa kwa kuachiana nafasi,” alisema. “Lakini kama ni tatizo, tutahitaji kufikiri upya namna ya kukaa kwa kuachiana nafsi na hilo litakuwa gumu.”

HATIMAYE kocha Dean Smith ameibuka na kubainisha jinsi nahodha wa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi