loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Covid-19 yaathiri wafanyakazi 5,000

ZAIDI ya wafanyakazi 5,000 katika sekta binafsi, ikiwamo hoteli za kitalii wameathirika na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unayosababishwa na virusi vya corona, huku wengine wakipoteza ajira kabisa.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wanawake, Wazee na Watoto, Maudline Castico, alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Aliwataka waajiri sekta binafsi ambao wamewapa likizo bila ya malipo wafanyakazi wao kuwafikiria na kuwapatia fedha za kujikimu kimaisha.

“Serikali inalifahamu tatizo ambalo limewapata wafanyakazi wengi katika sekta binafsi ikiwamo ya utalii huku hoteli nyingi zikiendelea kufungwa kutokana na janga hilo kuendelea duniani.”

''Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na mchakato wa kufanya tathmini kuhusu wafanyakazi wa sekta mbalimbali ambao wameathirika na corona. Tunawaomba waajiri wa sekta ya utalii kuwafikiria wafanyakazi waliopewa likizo bila ya malipo ili waweze kujikimu,'' alisema.

Baadhi ya asasi za kiraia zimeiomba serikali ya Zanzibar kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya utalii na makundi mengine ya wajasiriamali ili waweze kukabiliana na athari za mlipuko wa virusi vya corona ambazo zimewafanya kushindwa kufanya shughuli  zao.

Mkurugenzi wa asasi ya kiraia inayoshughulikia vijana ya Zanzibar Youth Forum (ZYF), Maulid Suleiman, alisema sekta ya utalii imeathirika  zaidi, ambapo vijana waliowekeza katika sekta hiyo wakiwamo wasambazaji wa vyakula hotelini na watembezaji wageni wamepoteza ajira kwa zaidi ya miezi minne sasa.

Alisema licha ya serikali kuruhusu kuanza tena kwa sekta ya utalii na kuingia kwa wageni nchini, bado hali haijawa nzuri kutokana na kwamba Ulaya maambukizi ya virusi vya corona bado yapo juu.

Akiwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021,Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, alisema wameanza kufanya tathmini za athari za ugonjwa wa covid-19 ambao umezorotesha shughuli za maendeleo kwa vijana na wajasiriamali.

Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, serikali imepunguza kodi za leseni kwa wafanyabiashara wadogo kama mama lishe ambapo sasa watalipa Sh 30,000 kwa mwaka na kupewa kitambulisho ambacho kitawawezesha kufanya biashara bila kubughudhiwa.

 

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi