loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Man U yampotezea ‘pacha’ wa Samatta

IMERIPOTIWA kuwa klabu ya Manchester United imepanga kuachana na dili la kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Jack Grealish, anayecheza pamoja na Mtanzania, Mbwana Samatta.

Hivyo kwa sasa timu hiyo imehamishia nguvu zake zote kwa mchezaji wa miamba ya Ujerumani, Borussia Dortmund, Jadon Sancho.

Kilichowafanya waachane na mchezaji huyo ni baada ya kuona hana thamani ya Pauni milioni 80 kama ilivyotajwa na Villa.

Mbali na sababu hiyo ya bei, lakini pia kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer, yupo kwenye mikakati ya kuijenga safu yake ya ushambuliaji, akipanga mbinu za kushambulia kutoka pembeni, hivyo Sancho ndiye anayeonekana kufaa.

Tayari Dortmund wameshatangaza dau la mchezaji huyo, amabpo timu itakayomtaka italazimika kutoa kitita cha Pauni milioni 110.

United bado haijasema lolote kuhusu dau hilo, lakini wachambuzi wengi wanaona kama watashindwa kutokana na klabu nyingi kuyumba kiuchumi kwa janga la ugonjwa wa covid-19.

United wanajipa moyo wa kumchukua Sancho, ambaye mkataba wake na Dortmund unamalizika mwaka 2022 baada ya kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.  

Hata hivyo, Dortmund imesema klabu yoyote inayomtaka mchezaji wao huyo ihakikishe inakamilisha taratibu za uhamisho kabla ya Agosti 10, ambapo itaanza maandalizi ya msimu mpya baada ya hapo hawatamuuza.

Kama dili hilo litagonga mwamba, Man United wanaweza kuhamia kwa Bayern Munich ili wamchukue kwa mkopo. Kingsley Coman.

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amewataka makocha wa timu ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi