loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wadau walivyonufaika uwepo wa Bodi ya Mikopo Sabasaba

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iliyoanzishwa katika utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliyezikwa jana, tangu kuanzishwa kwake imeendelea kuimarisha na kukuza ushirikiano na wadau wake.

Lengo la hatua hii ni kuwawezesha wanufaika wa mikopo kutambua wajibu na majukumu ya Bodi hiyo iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria ya HESLB (Sura ya 178). Hadi sasa Bodi imeshanufaisha watanzania zaidi ya laki nne.

Kulingana na sheria hiyo iliyoanzisha Bodi pamoja na mambo mengine, ina majukumu makuu mawili; la kwanza ni kutoa mikopo au ruzuku kwa wanafunzi wenye sifa na uhitaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na la pili ni kusimamia urejeshwaji wa mikopo hiyo kutoka kwa wanufaika kuanzia mwaka 1994/1995 Serikali ilipoanza kutekeleza sera ya uchangiaji elimu kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

BODI NA WADAU Ili kujenga uelewa wa pamoja baina yake na wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, Bodi imekuwa ikikutana mara kwa mara na wadau wake ambao baadhi yao ni waajiri, wanufaika na wananchi kwa ujumla kupitia maonesho, vyombo vya habari, mikutano na semina zinazolenga kujenga uelewa, kujibu hoja na kutoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kisheria ya Bodi.

Mwanzoani mwa mwezi huu unaoisha kesho, Bodi ilishiriki katika maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, barabara Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai Mosi hadi 13 mwaka huu.

Pamoja na kutoa huduma za papo kwa papo, Bodi pia ilieleza mikakati mbalimbali iliyojiwekea katika kusimamia utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa wanafunzi waliojiunga/wanaojiunga na taasisi na vyuo vya elimu ya juu nchini.

Katika maonesho hayo, Bodi iliweza kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya 1,300 ambapo wengi wao walikuwa wanufaika wa mikopo waliotembelea ban-Maendeleo (TASF) ambao pia umekuwa na jukumu la kusaidia kaya masikini.

Akizungumzia pengo la kuondoka kwa Rais Mstaafu Mkapa hasa wakati huu nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, Mjumbe wa Baraza la Taifa kwenye halmashauri ya CCM, Rajab Mwilima ambaye alifika kiwanjani hapo kutoa heshima zake, anasema chama kimempoteza nguli aliyetoa ushirikiano katika serikali zilizofuata baada yake ambayo ni ya awamu ya nne na hii ya sasa ya tano.

Wakati wananchi wakizungumzia matendo mema ya Mzee Mkapa, wengine waliokuwa wakiaga walishindwa kujizuia na kupatwa na mshtuko na kuzimia lakini timu ya huduma za afya ya dharura mkoani humo ilikuwa imejipanga na kuwahudumia.

Salima Matewele (86), mlemavu na mkazi wa Dumila mkoani Morogoro, naye alifika viwanjani hapo kutoa heshima zake za mwisho kwa Mzee Mkapa na kusema kiongozi huyo ni mdogo wake na kwamba amemsaidia kimaisha.

Matewele alisema hawezi kuacha kwenda kumuaga kwa sababu amefanya mambo mengi mazuri ndani ya nchi, kwa wananchi na kwa Chama Cha Mapinduzi. Dk Clement Kamage ni kiongozi wa kambi mojawapo zilizokuwepo viwanjani hapo kwa ajili ya kutoa huduma za dharura za afya kwa waombelezaji.

Yeye anasema wamehudumia watu wengi ambao walipatwa na mshtuko baada ya kuaga na idadi yao kwa siku tatu ilifika karibu wananchi 250.

Anasema ni msiba mkubwa ambao idadi kubwa ya waombolezaji ilijitokeza kutoa heshima zao na kwamba baadhi yao walipatwa na mshtuko na kuzimia wengine wakihitaji ushauri kisha baada ya muda kurejea katika hali ya kawaida.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alisema tujifunze kuishi na kuacha alama katika jamii ambazo hata tukifa zitaendelea kutumbuka, kauli aliyomaanisha kila mmoja atimize wajibu wake ipasavyo na kuwajibika huko kuwe na tija kwa familia, jamii na taifa ili hata tuondokapo matendo memo yabaki kuwa kumbukumbu mazuri na kuigwa na wengine.

Hakika Mkapa aliitendea mengi mema nchi hii na Afrika kwa ujumla kwani shehena ya sifa zake ikitawja ipasavyo, gazeti hili kutoka ukurasa wa kwanza hadi mwisho halitoshi.

Yatosha tu kusema, buriani Mzee Mkapa, mwendo umeumaliza, Imani umeilinda! da la HESLB na kufurahishwa na upatikanaji wa taarifa za papo hapo kuhusu kiwango cha makato ya deni la mkopo kwa wanufaika waliolipiwa na Serikali walipokuwa wakisoma katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu.

UTENDAJI NA HUDUMA KWA WATEJA:

Kutokana na mifumo imara ya usimamizi na ufuatiliaji iliyowekwa na Bodi, pamekuwa na maboresho katika utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na kuongeza ofisi za kanda ili kusogeza huduma kwa wateja.

Bodi ilianza ikiwa na ofisi Dar es Salaam pekee, lakini kwa sasa ina ofisi nyingine sita katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Mtwara na Zanzibar ambako inatoa huduma kwa wanafunzi wanaosoma katika taasisi za elimu ya juu, waajiri, wanufaika wa mikopo na wananchi wengine kwa ujumla.

Katika maonesho hayo ya Sabasaba, wananchi wengi walipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Bodi katika kuongeza idadi ya wanufaika wa mikopo kwa mwaka hususani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutoka wanufaika 98,300 mwaka 2014/2015 hadi wanufaika 132,392 mwaka 2019/2020 na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wahitaji wanaotoka katika familia maskini.

USHUHUDA WA WANUFAIKA:

Kufuatia mageuzi ya kimkakati yaliyofanywa na Bodi katika kuongeza makusanyo ya madeni na idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, wanufaika walikiri kuwa sehemu ya mafanikio hayo.

Wakati maonesho yakiendelea, mmoja wa wanufaika, Silvester Omary ambaye ni mtumishi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) aliguswa na jitihada hizo na kuamua kulipa papo hapo salio la mkopo wake alilokuwa anadaiwa na Bodi la Sh milioni 2.5 ili fedha hizo zitumike kusaidia wanafunzi wengine wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi kusoma.

Silvester alihitimu masomo yake ya Shahada ya Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza, mwaka mwaka 2013. Kwa hatua hiyo amekuwa ni kielelezo na mfano wa kuigwa kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kuhusu wajibu wa wanufaika kurejesha mikopo yao wanapohitimu masomo.

Silvester anasema mkopo wa fedha unaotolewa na Bodi umekuwa faraja kwa wanafunzi kutoka katika familia maskini ambao wengi walikuwa wamepoteza matumaini ya kusoma masomo ya elimu ya juu kwa kugharamia mahitaji yote kuanzia ada ya masomo, fedha za kujikimu, malazi pamoja na chakula hali inayowafanya wanafunzi husika kusoma kwa amani.

Silvester aliipongeza Bodi kwa jitihada zake katika kuwasaka na kuwabaini wanufaika wa mikopo, hivyo anatoa wito kwa wanufaika wengine kujitokeza kwa hiari na kurejesha mikopo ili iweze kuwanufaisha watanzania wengine wahitaji.

“Nilikuwa mnufaika wa fedha za Bodi nilipokuwa nasoma SAUT mwaka 2010- 2013, Bodi inatusaidia sana kwani ndio tumaini la maisha ya vyuoni katika kulipa ada na fedha za kujikimu.

Bodi imefanya watoto wengi kutoka familia maskini kama sisi kuweza kusoma,” anasema Silvester.

Mnufaika mwingine, Denis Kwame ambaye ni Ofisa Rasilimali Watu katika kampuni ya Cherry Garmet and Safety Solutions Ltd ya jijini Dar es Salaam alisema ofisi yake ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Bodi ili kuwezesha wafanyakazi wake kuanza kurejesha mikopo hiyo.

Aliongeza kuwa kutokana na kuguswa kwake na kasi ya ukusanyaji wa mikopo inayofanywa na Bodi, mwezi Februari mwaka huu alilipa mkopo wake wote wa Sh milioni tatu ikiwa ni fedha alizolipiwa na Serikali wakati alipojiunga na masomo ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1999 hadi 2002.

“Ofisi yetu ipo tayari tuanze kushirikiana kukusanya madeni ya mikopo ya Bodi.

Takribani shilingi milioni 10 zinatarajiwa kukusanywa na Bodi na wafanyakazi wetu wote wapo tayari kwa ajili ya kuanza kulipa madeni hayo kwani wengi wao ni wanufaika wa mikopo iliyowawezesha kusoma masomo yao ya elimu ya juu,’’ alisema Kwame.

MIKAKATI YA HESLB:

Kwa upande wake Ofisa Mikopo Mkuu wa Bodi, Tuli Madhehebi alisema ofisi yake imeendelea kutumia mbinu mbalimbali ili kuhamasisha umma katika urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu, ikiwemo kutumia maonyesho ya Sabasaba na kupata mafanikio makubwa kutoka kwa wadau wakiwemo wanufaika wa mikopo.

Anasema wakati wa maonyesho ya mwaka huu, Bodi ilitoa elimu kwa wanufaika kuhusu mbinu na njia mbalimbali wanazoweza kutumia kuanza kurejesha mikopo yao ili kuweza kukwepa adhabu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria kutokana na ama kuchelewa kuanza kurejesha au kutowasilisha makato ya mikopo ndani ya muda unaoruhusiwa.

“Tunaendelea kuwahamasisha wanufaika kutumia benki kwa ajili ya kununua madeni ya mikopo ya elimu kutoka Bodi.

Tuna barua maalumu ambazo tunawapa wanufaika wazipeleke katika taasisi za kifedha ili kuona namna bora ya kuwawezesha kurejesha mikopo yao ikiwemo kununua mikopo husika,’’ alisema Madhehebi.

Anaongeza kuwa Bodi pia ilitumia fursa ya maonesho hayo kutoa elimu kwa wanufaika wa mikopo ambao mara nyingi wamekuwa na malalamiko, maswali au maoni mbalimbali lakini wameshindwa kuyawasilisha katika mamlaka husika ikiwemo tozo ya kulinda thamani ya mkopo (VRF) inayokatwa kwa kiwango cha asilimia sita kila mwaka kutoka kwenye salio la deni.

Madhehebi anasema Bodi imeendelea kuwahamasisha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kutumia vyanzo mbalimbali vya kifedha walivyonavyo ili kuweza kumaliza mikopo kwa wakati na kujiepusha na adhabu zinazoweza kutolewa kwa mujibu wa sheria kwa ukiukaji wa taratibu za urejeshaji mikopo ya elimu ya juu.

Akizungumza katika Banda la Bodi wakati maonesho hayo yakiendelea, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi, Abdul- Razaq Badru alisema Ofisi yake imefanikiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni kutoka Sh bilioni 30 mwaka 2014/2015 hadi Sh bilioni 192.9 mwaka 2019/2020 na kuiwezesha Serikali kusomesha idadi kubwa zaidi ya wanafunzi wahitaji wenye sifa za kujiunga vyuo vikuu.

Badru pia aliwapongeza pia wanufaika binafsi waliorejesha mikopo yao waliopatiwa na Bodi.

Ni dhahiri kuwa wigo wa utoaji elimu ya juu nchini unaendelea kupanuka, na hivyo, ili kulinda ubora wa elimu hiyo Bodi ya Mikopo itaendelea na jukumu la kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu ili fedha hizo ziweze kukopeshwa kwa wanafunzi wengine wahitaji.

 

Mwandishi ni Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo. Mawasiliano yake: ingayonga@ heslb.go.tz

TAIFA la Tanzania hivi karibuni lilipita katika majonzi makubwa ya ...

foto
Mwandishi: Ismail Ngayonga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi