loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KOCHA WA YANGA MAKUBWA YAMKUTA

CHAMA cha Soka cha Afrika Kusini (SAFA) kinakusudia kumzuia kocha wa Yanga Luc Eymael kurejea na kufanyakazi tena nchini humo.

Eymael alitimuliwa na vigogo wa soka Tanzania Yanga Jumatatu baada ya kutoa matamshi ya kibaguzi nchini na kulalamikia klabu hiyo kutomuhudumia na kusababisha mashabiki wa soka nchini kumjia juu katika mitandao ya kijamii.

Wakati akitetewa na wakala wake na yeye mwenyewe akijitetea kuhusu kuwa mbaguzi, SAFA imechuka hatua kubwa kwa kuonesha mshikamano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la kulalamika kwa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kuhusu kitendo cha kocha huyo.

Katika mtandao wao rasmi, SAFA ilithibitisha kuwa imechukua hatua kuandika barua kwa Waziri wa Michezo kuelezea nia yao hiyo ya kumfungia kabisa kocha huyo kufanya kazi nchini humo, imesema kuwa SAFA imeshauri kocha huyo asipewe kabisa kibali cha kufanyakazi nchini humo.

Pia imelipeleka suala hilo Fifa, pamoja na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kumchongea kocha huyo na kunesha mshikamano na TFF na kuihakikishia ushirikiano katika hatua yoyote watakayochukua. Taarifa hiyo iliendelea:

“Bahati mbaya hali hii imejitokeza wakati kuna kampeni kubwa ya dunia kupinga masuala ya ubaguzi.

Afrika ina uzoefu na suala hili la kiubaguzi baada ya watu wake kuchukuliwa utumwa na kupelekwa katika mabara mengine.”

Huenda leo hii angekuwa nyota wa muda ...

foto
Mwandishi: JOHANNESBURG, Afrika Kusini

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi