loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea ubunge mbaroni, Gambo achunguzwa

Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Arusha, imekiri kuwakamata wagombea 20 mkoani Arusha, akiwemo mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeoomba kugombea ubunge, Philemon Mollel.

Kaimu Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, James Ruge aliwaeleza waandishi wa habari kuwa pia walipokea taarifa za tuhuma za kutoa rushwa zinazomhusu mwanachama mwingine wa CCM aliyeoomba kugombea ubunge Arusha Mjini, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Ruge pia alikiri kuwa Takukuru hadi sasa bado wana simu mbili za mfanyabiashara Mollel, lakini yeye ameachiwa kwa dhamana.

Katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni, mtuhumiwa huyo, Mollel alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 68. Gambo aliongoza kwa kupata kura 333 na nafasi ya tatu ilishikiliwa na Albert Msando aliyepata kura 22.

Ruge alisema kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu waliokamatwa na waliotolewa taarifa kuhusu tuhuma za kutoa rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni za ubunge na udiwani na ukikamilika wafikishwa mahakamani. Alisema kuwa Takukuru ilipokea taarifa za tuhuma za Gambo kujihusisha na vitendo vya kutoa rushwa katika kipindi cha kura za maoni na bado inaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha.

“Ni kweli taarifa za Gambo kujihusisha na kutoa rushwa tunazo ofisini na tunaendelea kuzifanyia kazi na sio yeye pekee yake wapo wanasiasa wengine 20 taarifa zao bado tunaendelea kuzichunguza na tukikamilisha tutawafikisha mahakamani” alisema Ruge.

Ruge alikanusha kwamba taasisi hiyo imeshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa rushwa za kisiasa ambao ni wafuasi wa CCM, kwa madai kwamba chama hicho kimetoa maelekezo kwamba taarifa za watuhumiwa hao zipelekwe ofisini.

Alisema kuwa chombo hicho hakifanyi kazi kwa kufuata maelekezo ya mtu ama chama cha siasa, bali kinafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria.

Alisema kuwa watuhumiwa wengine 20 wa kisiasa kutoka wilaya za mkoani Arusha, waliokamatwa na Takukuru wakijihusisha na vitendo vya rushwa, watafikishwa mahakamani iwapo watathibitika kuhusika na vitendo hivyo.

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi