loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tshishimbi awaaga mashabiki Yanga

WAKATI siku 14 alizopewa, Papy Tshishimbi, kusaini mkataba zikikaribia kumalizika na hajatekeleza hilo, ameibuka na kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.

Akizungumza na HabaLeo jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick, alisema mchezaji huyo alipewa ofa na klabu hiyo na alitakiwa kusaini ndani ya siku 14, lakini hadi sasa siku saba zikiwa zimesalia bado hajafanya hivyo na kuongeza kuwa, kama hatasaini katika muda uliopangwa klabu itatafuta mbadala wake.

Akizungumza Dar es Salaam jana Tshishimbi ambaye mkataba wake unamalizika kesho kutwa, alisema amekaa kwenye timu hiyo kama familia, hivyo amewaomba mashabiki kumtakia kila la heri kama kuthamini mchango wake.

“Nimepewa mkataba, lakini hata hivyo sijasaini kwa sababu sijaridhika na kiwango cha fedha wanachotaka kunipa, nimewaomba waongeze lakini wanashindwa kuongeza, hivyo nimeona niwaage mashabiki kwa kuwa nimekaa kwenye timu kama familia, endapo uongozi utanihitaji nibaki tutaongea wala haina shida,” alisema Tshishimbi.

Naye Wakili Patrick alisema kwa sasa timu hiyo inamambomengi ya kufanya ikiwamo kusuka upya benchi la ufundi baada ya kumfukuza kocha Luc Eymael na kama mchezaji huyo hatafanya kulingana na ofa aliyopewa, klabu haitakuwa na muda wa kumfutilia tena.

Kabla ya sakata hilo la mkataba kipindi cha dirisha dogo, Tshishimbi alikuwa akihusishwa kujiunga na Simba ambao kwa sasa wanaonekana hawana mpango naye kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Tshimbimbi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alijiunga Yanga akitokea Mbabane Swallows na Yanga walimwona katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Azam FC.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi