loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SVEN: TUNAIHESHIMU NAMUNGO

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema kwa sasa anawaandaa na kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Namungo, unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, mkoani Rukwa.

Fainali hizo za tano za ASFC, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Akizungumza kutoka Mbeya jana, Sven alisema jambo muhimu analolipa kipaumbele kama kiongozi wa benchi la ufundi ni kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia, pamoja na kukabiliana na mazingira ya uwanja watakaoutumia.

“Jambo muhimu ni kujiandaa kisaikolojia na maandalizi yanakwenda sawasawa na lengo letu ni kushinda mchezo na kuvaa medali za dhahabu na kutengeneza historia ya kujiongezea mataji kuwa mawili msimu huu,” alisema Sven.

Alisema siyo mchezo rahisi kama baadhi ya watu wanavyotabiri kuwa kikosi chake kitabeba ubingwa huo, hivyo Namungo wanastahili kupewa heshima kwa kuwa hadi kufika kwenye hatua hiyo wamepambana na wamefanya kazi kubwa kushinda mechi zote zilizopita.

Pia Sven amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono kwa kushangilia kama ilivyo kawaida yao ili kuongeza morali kwa wachezaji wakiwa uwanjani kutimiza majukumu yao ipasavyo wakijua wana deni la kuwalipa .

Wakati huohuo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kufika Rukwa leo kitokea Mbeya na tayari nyumba za kulala wageni mjini humo zinaripotiwa kujaa.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    Ibrahim
    31/07/2020

    Naitakia timu yangu Simba kila la kheri kwa mechi hii na nyingi miaka ijayo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi