loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ni vita kupanda, kushuka

MICHEZO ya marudiano na ya mwisho ya mchujo `Play-Off’ kutafuta timu mbili zitakazoungana na zile 16 kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara inafanyika leo wakati Mbeya City itawaalika Geita Gold ya Ligi Daraja la Kwanza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Wakati huo mchezo wa pili utazikutanisha Mbao FC ya Ligi Kuu, ambayo itawakaribisha Ihefu FC ya Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Michezo hiyo inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na matokeo ya mechi zilizopita, ambapo Mbeya City ilifungana bao 1-1 dhidi ya Geita Gold wakati Ihefu iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Mbao FC na kila kikosi kimedhamiria kushiriki Ligi Kuu msimu ujao,

Ihefu na Mbeya City, zote zinatoka kwenye mkoa mmoja walianza vizuri licha ya Mbeya City kuanza kwa sare lakini wako katka nafasi nzuri, kwani walipata bao ugenini, hivyo wanahitaji sare yoyote au ushindi ili kuendelea kuwepo Ligi Kuu msimu ujao.

Kocha wa Mbeya City, Amri Said ametamba kikosi chake kumaliza kazi kwenye mchezo huo kwa kuwa watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wakichagizwa na mashabiki wao, ambao wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo dhidi ya Geita Gold.

“Tulifanya kazi kubwa kwenye mchezo wa ugenini na kufanikiwa kupata pointi moja, lakini mechi ya kesho (leo) tunatakiwa kumaliza kazi kwa kupata ushindi  jambo ambalo linawezekana kwa kuwa mashabiki wetu watajitokeza kutushangilia,” alisema Said.

 

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi