loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Namungo yataka kuonesha maajabu

TIMU ya soka ya mkoani Lindi, Namungo imesema inataka kuwaonesha Watanzania kile inachoweza kufanya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) dhidi ya Simba utakaochezwa kesho.

Mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Namungo itacheza fainali hiyo kwa mara ya kwanza, huku Simba ikicheza kwa mara ya pili baada ya kufika msimu wa 2016/2017, ambapo iliifunga Mbao mabao 2-1 na kuchukua taji hilo.

“Tumejipanga vizuri kwa ajili ya fainali, ninaamini tutaweka historia mpya na kuwaonesha Watanzania kile tunachoweza, muhimu tunaomba watu watuunge mkono,”alisema mchezaji wa timu hiyo, Bigirimana Blaise.

Kocha wa Namungo, Thiery Hitmana alisema kikosi chake kinaendelea vizuri na amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake kinachohitajika kufanya kufikia malengo waliyojiwekea ya kuchukua taji hilo kwa mara ya kwanza.

Alisema wachezaji wengi ni mara yao ya kwanza kucheza fainali hiyo, hivyo wanataka kuacha historia mpya.

Hitimana alisema anajua wapinzani wao Simba ni timu kubwa na wanawaheshimu ila wao watakuja na mbinu zao walizoanza nazo tangu kuanza kwa msimu huu.

Fainali hiyo inachezwa mkoani humo kwa mara ya kwanza ikiwa ni mpango wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupeleka michezo mikubwa mikoani kuhamasisha michezo hasa katika mikoa iliyoko chini kisoka.

Fainali ya kwanza kupelekwa mikoani iliwakutanisha Simba dhidi ya Mbao jijini Dodoma, kisha ikafuata ya Mtibwa dhidi ya Singida United iliyochezwa mkoani Arusha na hii inayofuata ni ya tatu.

Kwa upande wa Simba walioweka kambi mkoani Mbeya kujiandaa na mchezo huo, tayari wamewasili Rukwa huku Meneja wa kikosi hicho Abbas Ally akisema kila kitu kiko sawa, vijana wake wana morali ya kutaka kuchukua kombe hilo kwa mara ya pili.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi