loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Minziro aahidi kubaki Ligi Kuu

KOCHA Mkuu wa timu ya Mbao FC, Fredy Minziro ameahidi kuhakikisha anashinda mchezo wake wa leo dhidi ya Ihefu FC ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) katika mchezo wa hatua ya mtoano (Play off) utakaochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba leo.

Akizungumza jana Minziro alisema timu yake ilipoteza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-0 Jumatano kwenye Uwanja wa Highland Estate wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Alisema wamerekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri.

"Tulipoteza mechi yetu ya kwanza, tumejipanga vyema pamoja na vijana wangu jambo la muhimu kwetu ni kuhakikisha tunashinda mechi yetu kwa mabao matatu na kuendelea ili tuweze kubakia katika Ligi Kuu,’’ alisema Minziro.

Kocha huyo wa zamani wa Yanga, Alliance FC na Singida United alisema anawaomba wadau na mashabiki wa soka mkoani Mwanza kujitokeza kwa wingi leo kuishangilia timu yao ifanye vyema katika mchezo wa leo.

Nahodha wa Mbao FC, Wazir Junior alisema mchezo wa leo kwao ni fainali na mchezo muhimu sana kwa kuwa timu yao ilipambana sana mpaka kufika hatua ya mtoano.

Alisema hawajakata tamaa bali watapambana kuweza kushinda mabao matatu na kuendelea ili waweze kubakia katika Ligi Kuu msimu ujao.

 

 

PAZIA la Ligi Kuu ya soka ya Wanawake ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi