loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lampard ataka kuipa Chelsea FA Cup

OCHA wa Chelsea, Frank Lampard ameweka nguvu zake katika kumaliza vizuri msimu wake wa kwanza kama kocha wa timu hiyo kwa kuiongoza the Blues kutwaa taji la Kombe la FA.

Chelsea leo inashuka dimba la Wembley kucheza dhidi ya Arsenal katika mchezo wa fainali.

Lampard amefurahia kushinda fainali nne wakati akiwa mchezaji wa Chelsea, lakini mikono yake kushika taji lake hilo la kwanza katika kipindi chake cha ukocha, itakuwa na umuhimu mkubwa kwake.

Kocha huyo ana umri wa miaka 42 tayari ameiwezesha Chelsea kufusu moja kwa moja kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza ndani ya nne bora katika Ligi Kuu.

Katika taarifa yake kwa Lampard, huo ni msimu wake wa pili kama kocha, aliiwezesha timu hiyo kufanya vizuri licha ya kuichukua katika hali mbaya miezi 12 iliyopita.

Wakati Lampard alipowasili Stamford Bridge Juni mwaka 2019 baada ya msimu mmoja wa kuifundisha timu ya Daraja la Pili ya Derby, amekuwa akiungwa mkono na mashabiki, ambao walimshuhudia akiichezea timu hiyo kwa miaka 13.

Lakini watabiri wengi wa soka walikuwa na wasiwasi sana kama Lampard alikuwa mtu sahihi kuirejesha Chelsea katika mstari baada ya kipindi cha kocha Maurizio Sarri.

"Kulikuwa na mambo mengi yasiyojulikana wakati nikitua hapa, tunaweza kwenda mbele bila ya Eden Hazard? Tunajua tumempoteza mchezaji mkubwa na muhimu,"alisema Lampard.

"Ndani ya kundi kuna moy na sasa ni juhudi za timu."

Kwa jitihada zake wakati Chelsea imefungiwa kusajili, Lampard aliwatumia wachezaji chipukizi wa klabu hiyo na kuwapa nafasi ya kudhihirisha thamani zao.

 

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amewataka makocha wa timu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi