loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Mameneja Tanroads Lindi, Pwani watumbuliwa

 

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Issac Kamwelwe ametengua uteuzi wa meneja wawili wa Wakala wa Barabara (Tanroas) wa Mikoa ya Lindi na Pwani kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ya kusimamia miundo mbinu ya barabara kwenye maeneo yao. 

Uamuzi huo wa Waziri Kamwelwe umefanyika ikiwa ni siku moja tangu Rais John Magufuli alipopita kwenye barabra za mikoa hiyo akitoka mkoani Mtwara kuhudhuria maziko ya Rais mtaaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kukerwa na uharibifu mkubwa wa barabara za mikoa hiyo.

Kamwelwe alichukua uamuzi huo jana alipokuwa akikagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye kilometa 1.6 inayotoka Kibaoni kwenda Makao Makuu ya Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi.

Alikuwa njiani kutoka Mji Mdogo wa Inyonga uliopo wilayani Mlele kwenda mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Waziri Kamwelwe, mameneja aliotengua uteuzi wao ni Issac Mwanawima, Meneja wa Lindi na Yudas Msangi aliyekuwa Kaimu Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Pwani.

Waziri Kamwelwe alisema Rais Maguguli alipita juzi kwenye barabara  hizo na kushuhudia lami ikiwa imeharibika na barabara imekuwa kama  ya vumbi wakati zipo fedha za matengenezo kupitia Mfuko wa Barabara zipo.

Alisema Tanroads walikuwa na sifa nzuri  lakini wameanza kuharibiwa na watumishi wachache. “Kwa hiyo watambue kuwa kipindi hiki siyo cha  kufanya mchezo kila anayebainika kushindwa kutekeleza majukumu yake atambue kuwa atawajibishwa,” alisema. 

Aliwataka mameneja wa Tanroads kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu barabara zote zilizoharibiwa na mvua za msimu huu zinakarabatiwa  na zinakamilika. 

Akifafanua, Kamwelwe alisema wizara yake imetoa zaidi ya Sh bilioni 35 kwa matengenezo ya barabara hizo na kwamba meneja atakayeshindwa kukamilisha, ajihesabu kuwa umeneja wake utaishia tarehe hiyo. 

Alisema kabla ya kutoa agizo, aliwaita mameneja wa Tanroads wa mikoa yote kwenye kikao  kilichofanyika jijini Dodoma na kuwaelekeza wahakikishe wanafanya matengenezo ya barabara zote zilizoharibika kwa mvua za masika.

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Mpanda

3 Comments

 • avatar
  pius ngalasoni
  01/08/2020

  Huyu Waziri wa Ujenzi alikuwa nasubiri Rais apite ndo amkumbushe wajibu wake .kwa mini Haiti kukagua barabara ilhali ana wasaidizi wawili . Nae ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia kazi zake.

 • avatar
  pius ngalasoni
  01/08/2020

  Huyu Waziri wa Ujenzi alikuwa nasubiri Rais apite ndo amkumbushe wajibu wake .kwa mini Haiti kukagua barabara ilhali ana wasaidizi wawili . Nae ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia kazi zake.

 • avatar
  Godo Biwi
  01/08/2020

  Hiyo ni haki yao haswa huyo wa Mkoa wa pwani.Previous RM Eng Sarakikya was tough on corrupted official and member of staff.Alivyoingia huyo Yudas Msangi,,aliwakumbatia.Sasa wamemuangusha.mfano HWBU wa sasa is the most corrupted senior staff pale,amemkumbatia na huyo HWBU amekuwaa anatumia mikataba kuwaondoa wale staff ambao the best kwenye kulinda barabara na kukumbatia wala rushwa wenzake.Sasa Eng Msangi amevuna alichopanda.Mungu amesikia kilio cha wanyonge.Thank u Mr President, JPM

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi