loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mufti apongeza Watanzania walivyojitokeza kumuaga Mkapa

MUFTI wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir amewapongeza Watanzania kwa namna walivyojitokeza na kushiriki kikamilifu katika msiba wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliyezikwa wiki hii kijijini kwake Lupaso wilayani Masasi katika Mkoa wa Mtwara. 

Zubeir alitoa pongezi hizo jana kwenye Baraza la Idd el Haji lililofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi. 

Alimtaja Mkapa kuwa ni kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kujali maisha ya Watanzania wote bila ubaguzi hadi kufikia uamuzi wa kutoa majengo ya serikali na kuwakabidhi yakafanywa kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu. 

Alisema ni kiongozi aliyeivusha Tanzania na kuifanya kuwa na maendeleo makubwa kabla ya kukabidhi kwa Rais Jakaya Kikwete. Aliwataka Watanzania kuendelea kumuombea dua apate pumziko lenye amani.

Baraza hilo lilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam,  Abubakar Kunenge na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini. 

 

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi