loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ole Sendeka aaga Njombe, akabidhi ofisi

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Njombe,  Christopher ole Sendeka amewataka wataalamu wa ujenzi wa barabara, madaraja na    majengo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Amewataka wabadilike kwa kuwa Mkuu mpya wa mkoa aliyeletwa badala yake baada ya yeye kugombea ubunge jimboni kwao Simanjiro, Manyara ni mtaalamu wa ujenzi.

Ole Sendeka alitoa mwito huo wakati akikabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo. Alisema yeye alifanya kazi kwa kuuliza wataalamu wa ujenzi lakini si RC huyu mhandisi kitaaluma.

"Mmeletewa Mhandisi Marwa Rubirya. Huyu hamtacheza naye iwe barabara za TARURA, za TANROADS au ujenzi majengo yoyote. Huyu hamtamdanganya,Ole Sendeka aliwaambia.

Ole Sendeka amekabidhi hundi ya shilingi bilioni tano ambazo ni fedha zilizookolewa kutoka waliofuja fedha za Benki ya Wananchi Njombe (Njocoba) na vyama vya ushirika.

"Hii ni hundi ya shilingi bilioni 5.397 ya fedha za wananchi ambazo zimerejeshwa baada ya Rais John Pombe Magufuli kuagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wote waliochukua fedha za vyama vya ushirika, vyama vya msingi na Saccos wazirudishe. Namkabidhi RC mpya ili akaweke utaratibu wa kuzigawa fedha hizi," aliongeza Sendeka.

Katibu Tawala mkoa wa Njombe, Catarina Revocat alisema Ole Sendeka alikuwa kiongozi wa mfano kwa kuongoza watendaji wake wote kwa kuzingatia maelekezo yake anayoyatoa na kuyafanyia kazi kikamilifu.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, RC mpya, Marwa Rubirya alisema anatarajia kuona viongozi wa wilaya na halmashauri wanakuwa wa kwanza kutatua changamoto za wananchi kabla hazijamfikia.

"Tuna wajibu kusaidia wananchi kutatua kero zao. Mwananchi akishindwa kutatuliwa kero anasononeka.  Nitashangaa kero zilizotokea katika wilaya mpaka anayelalamika aipeleke kwa mamlaka za juu," alisema RC Rubirya.

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: Emmanuel Octavian, Njombe

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi