loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Waislamu watakiwa kutii serikali

WAUMINI wa dini ya Kiislamu wametakiwa  kuyaishi maagizo ya Mtume Muhammad aliyowaachia kuitii na  kuiheshimu serikali yao.

Akizungumza jana Arusha kuadhimisha ibada ya Sikukuu ya Idd el Hajj, Shehe wa mikoa  ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, Shafi Muhammad alisema asiyeitii na kuheshimu serikali anaenda kinyume Mtume Muhammad. 

Alisema kila mmoja ni vema akajitahidi kuishi vizuri na kuwa mfano katika jamii katika mazingira  yoyote anayokumbana nayo.

"Tiini Taifa  bila shuruti  na msipingane na serikali yenu kwa maana kwenda kinyume na sheria za nchi na mtume wetu ambaye alitueleza  na kutufundisha juu ya  mapenzi kwa nchi  kwani ni sehemu ya imani," alisema.

Alihimiza kusaidia watu wasiojiweza ili kila mtu apate thawabu mwisho wa maisha duniani.

Shehe Shafi alisema kuwa endapo kila Mwislamu ataishi na kufuata mafundisho ya Mtume Muhammad,  nchi itakuwa tulivu. 

Sikukuu ya Idd  Ul Adhha au Idd ya kuchinja huadhimishwa baada ya kumalizika kwa Ibada ya Hija, nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu.

Mkuu wa Wilaya, Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi