loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanufaika Tasaf kufanyiwa uhakiki

SERIKALI inakusudia kufanya uhakiki wa kaya zote za wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini (Tasaf) awamu ya tatu ili kuondoa walengwa hewa na waliopoteza sifa kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mpango huo.

Katika ujumbe aliotuma kwenye Halmashauri ya Itigi ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga aliwaambia wajumbe wa kikao kazi cha wakuu wa idara na mafunzo ya wawezeshaji kuwa safari hii umakini wa hali ya juu unatakiwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

“Mtakumbuka hapo nyuma kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu mpango huu kuwa na watu wasiostahili, wakiwemo watu wasio masikini, viongozi, watu waliohama au waliofariki ambao hao wote waliitwa walengwa hewa,” alisem. 

Aliongeza kuwa wakati wa uzinduzi wa kipindi cha pili,  Rais John Magufuli aliagiza kwamba kabla ya shughuli zozote, uhakiki wa walengwa ufanyike kote nchini ili kuondoa kaya zote za walengwa ambazo zimepoteza sifa.

Alisema kuwa ili kutekeleza agizo la Rais na pia kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii ya kuwemo walengwa hewa, utekelezaji utaanza kwa kusafisha daftari la walengwa. 

“Kuna viapo vya uadilifu ambavyo kila mshiriki wa mafunzo haya atatakiwa kusaini. Viapo hivyo visichukuliwe kama ni utaratibu tu. Vitatumika kuwajibishana itakapogundulika katika eneo ambalo utaenda kufanyia kazi kutabainika bado zipo kaya ambazo zinatakiwa kuondolewa,” alifafanua.

Alieleza kuwa baada ya kukamilika kipindi cha kwanza cha mpango huu, serikali iliamua kuendelea na kipindi cha pili ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi wa Serikali kupitia Tasaf kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umasikini.  

Alisema kuwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) kitatekelezwa katika halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na wilaya zote za Zanzibar ambapo kaya milioni 1.45 zenye jumla ya watu zaidi ya milioni saba kote nchini zitafikiwa, ikiwa ni nyongeza ya kaya laki tatu na nusu.  

Aidha, alisema kuwa mkazo mkubwa katika kipindi cha pili utawekwa katika kuwezesha kaya zitakazoandikishwa kufanya kazi ili kuongeza kipato, kuhakikisha huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa na kuendeleza raslimali watoto, hususan katika upatikanaji wa elimu na afya.  

Takwimu zinaonesha kwamba utekelezaji wa Mpango wa Tasaf kipindi cha kwanza, uliweza kufikia walengwa asilimia 70 tu nchi nzima ambapo umechangia kupunguza umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya kwa asilimia 10 na umasikini uliokithiri kwa asilimia 12 kwa kaya maskini sana. 

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Itigi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi