loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Awamu ya tatu Tasaf kutekelezwa kwa mtandao

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), awamu ya tatu umeanza kutekeleza kipindi cha pili, sambamba na kutoa ruzuku za walengwa wake kwa njia mfumo wa mtandao nchi nzima.

Aidha uhakiki wa wanufaika wa mfuko ambao ni kaya masikini utafanyika kieletroniki, lengo likiwa kuwafuta kwenye orodha wanufaika hewa ambao wengine ni marehemu.

Hayo yalibainishwa katika hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga iliyosomwa kwa niaba yake na Josephine Pupia kwenye ufunguzi wa kikao kazi kilichojumuisha wakuu wa idara kuhusu utekelezaji wa mfuko huo awamu ya tatu na uhakiki wa kaya maskini.

Kikao hicho kilifanyika katika halmashauri ya Nsimbo iliyopo katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Aliongeza kusema kuwa katika utekelezaji wa Tasaf awamu ya pili vijiji katika halmashauri 185 nchini vilifikiwa na mfuko huo.

“Utekelezaji wa Tasaf awamu ya tatu utafanyika katika vijiji, mitaa na sheiha zote nchini Tanzania Bara na Visiwani na kujumuisha maeneo ya vijiji, mitaa na shaiha ambayo hayakufikiwa na mfuko katika kipindi chs utekelezaji wa awamu ya kwanza na ya pili... Tasaf katika kipindi chake cha awamu ya tatu kinatarajia kuzifikia kaya masikini milioni saba nchini ikiwa ni ongezeko la kaya 300,500,” alieleza Mwamanga katika hotuba yake.

Mwezeshaji wa mafunzo, Deogratius Dingona alieleza kuwa madhumuni ya mfuko  huo katika kipindi cha pili cha utekelezaji wa awamu ya tatu ni kuziwezesha kaya masikini kujiongezea kipato na kuboredha  huduma za kijamii ikiwemo afya, maji na elimu na pia wanufaika wawekeze katika kuendeleza watoto wao kielimu kwa kuwapeleka shule.

Mratibu wa Tasaf, Halmashauri ya Nsimbo iliyopo katika Wilaya ya Mpanda, Alex Magesa alisema kazi ya uhakiki wa kaya masikini inaendelea katika halmashauri hiyo ili kuwabaini wanufaika hewa.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Mpanda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi