loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ashauri Wizara ya Fedha, BoT kusaidia wakopeshaji

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutuba ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuratibu kwa karibu vikundi vinavyotoa huduma ndogo za fedha vikiwemo Vikoba ili kutoa elimu na ufahamu kabla ya mwananchi kujiunga au kukopeshwa fedha ili kuwa na uhakika na usalama wa fedha zao.

Tutuna alitoa rai hiyo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu.

“Kuna vikundi vinavyowaambia wananchi kuwa vinatoza riba ya asilimia tano, kumbe asilimia hiyo ni kwa mwezi na sio kwa mwaka ukifanya hesabu utagundua riba kwa mwaka ni asilimia 60 ilihali kuna benki zinazotoa mikopo kwa riba ya asilimia 18 kwa mwaka, hivyo lengo la huduma ndogo za fedha kumsaidia mwananchi kurahisisha shughuli za kiuchumi halifikiwi,” alieleza.

Tutuba alisema kuwa kuna vikundi wananchi wanaunganishwa bila kuwa na ufahamu wa kutosha hivyo kuchangishwa fedha lakini akienda kudai maslahi yake anaambiwa fedha hazipo, jambo ambalo taasisi zinazodhibiti vikundi hivyo zinabidi kufuatilia kwa karibu kwa kutoa elimu toshelevu ili mwananchi aweze kufanya maamuzi sahihi.

Alisema pia kuwa kwa ngazi ya halmashauri anashauri fedha zinazotolewa kama mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu, zitolewe kwa mfumo wa kibenki utakaosaidia ufuatiliaji na urejeshwaji wa mikopo hiyo kwa urahisi kwa kuwa na uelewa wa maana ya mikopo.

Tutuba alisema kuwa kuna vikundi ambavyo vinaanzishwa kwa mtazamo wa kutafuta fedha bila kuwa na wazo au biashara yenye tija kwa kikundi na eneo alipo hivyo dhana ya kuwakomboa wananchi kupitia mikopo hiyo kutofikiwa.

“Wale wanaokopeshwa wakipata fedha katika mifumo ya kibenki watapata elimu inayotakiwa, watarejesha fedha kwa uhakika, watafuatiliwa lakini hata dhamana sio lazima ziwe za ajabu zaidi ya muhtasari wa Kijiji kutambua biashara yake,” aliongeza.

Alisema ikiwezekana ianzishwe Benki katika Serikali za Mitaa itakayosaidia kutoa fursa kwa watu kutoa wazo la mradia au biashara na litakapodhibitishwa lina tija katika uchumi wa Kijiji au Kata linaweza kudhaminiwa na serikali ya kijiji ili watu waweze kurejesha fedha.

Alifafanua kuwa benki hiyo itawahudumia wananchi kwenye maeneo yao badala ya kuwaacha wananchi kwenda kurubuniwa kwenye vikundi vyenye dhamira ovu.

Mtaalamu wa Masuala ya Sekta Ndogo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Joseph Msumule alisema kuwa Sheria mpya ya huduma ndogo za fedha imeanzishwa ili kurahisisha utoaji wa huduma hiyo lakini kudhibiti wafanyabiashara wenye nia ovu kwa wananchi, pia sheria imeweka kiwango cha mtaji kwa wakopeshaji ili kusajiliwa, lengo likiwa ni kusaidia vikundi vya kuweka na kukopa kuwa na uwezo wa kutoa huduma wakati inahitajika.

 WAZEE na watu wanaoishi katika mazingira magumu wapatao 200 wanaoishi na kulelewa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), kata ya Chang'ombe jiji la Dodoma wamepatiwa misaada mbalimbali ili kuwawezesha kujikimu Misaada hiyo ni pamoja na mbuzi 50 wenye thamani ya Sh 3,000,000 kwa ajili ya wajane, wazee na wanaoishi katika mazingira magumu.

Misaada hiyo imetolewa na Taasisi ya Dar- Ul- Muslimeen yenye makao yake Dodoma. Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya wazee hao, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Ajira, Kazi na Vijana, Athony Mavunde pamoja na kushukuru taasisi hiyo alisema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi na makampuni binafsi kwa kusaidia jamii ya watu wenye mahitaji.

Mavunde alisema kuwa serikali inatambua juhudi hizo zinazofanywa na taasisi na makampuni binafsi katika kuhakikisha jamii yenye kuhitaji mahitaji maalumu kama vile ya kielimu, afya, chakula na mavazi wanafikiwa kwa lengo la kutatua changamoto zao wanazokabiliana.

“Hivyo basi nitoe rai kwa taasisi na makampuni watu binafsi ziige mfano kwa taasisi ya Dar-ul-Musilmeen chini ya mkurugenzi wake, Muslimu Bhanji, ambaye mara zote amekuwa akijitoa kwa ajili ya kusaidia watu wenye mahitaji, lakini sivyo hivyo tu hata watu wenye mishahara mikubwa na kipato wanaweza wakafanya hivyo,” alisema.

Aidha katika hatua nyingine Mavunde pia aliwataka watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi kuliombea Taifa ili Mungu aweze kuwapitisha viongozi watakaotokana na chaguo lake ambao watasiammia maslahi ya taifa na kuilinda amani iliyopo.

Bhanji alisema kuwa sadaka hiyo imetolewa kwa ajili ya kusaidia jamii isiyojiweza katika kata hiyo ya Chang'ombe wakiwemo wajane, yatima,wazee na watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Tabora, Seraphina Nsana akiwaapisha Waratibu wa Mikoa na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka mikoa ya Kigoma na Tabora jana wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika mkoani Tabora ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao. 

“Tumia teknolojia za kilimo na utawala bora kwa ukuaji wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi