loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kabudi ‘akunwa’ teknolojia ya kilimo cha mjini, vijijini

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi ametembelea banda la Kinondoni katika maonesho ya wakulima ya nanenane mkoani hapa na kupongeza kwa kuwa na vitu ambavyo vinavutia watazamaji.

Profesa Kabudi akiwa katika banda hilo, alieleza kuvutiwa na Teknolojia ya Kilimo cha Mjini na Vijijini ikiwemo kilimo cha kisasa cha mbogamboga na mazao ya chakula sambamba na ufugaji wa kisasa.

Aliongeza kuwa kupitia maonesho hayo, wananchi wa Dar es Salaam wana kila sababu ya kujifunza teknolojia hizo kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa kuwa itawawezesha kuendesha shuguli zao za kilimo cha mijini.

Alisema katika banda hilo pia amevutiwa na wajasiriamli wanawake wanaotengeneza bidhaa za nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambao inaongeza thamani ya bidhaa hiyo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuwawezesha wajasiriamali hao.

“Mkurugenzi nakupongeza wewe pamoja na timu nzima ya Kinondoni, mmefanya kazi kubwa kwenye maonesho hayo, mmewaletea wananchi mambo mazuri na wanapokuja kuangalia wanaondoka na ujuzi mzuri katika nyanja zote ikiwemo kilimo, ufugaji, usindikikaji wa vyakula na utengenezaji wa bidhaa za nguo za batiki,” alisema.

Aidha aliipongeza manispaa hiyo kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo viatu na kusema kuwa mpango huo ni mzuri kwani unaendana sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya Viwanda ya Rais John Magufuli.

Aliongzea kuwa Rais Magufuli anaguswa na vijana ambao wanatumia ujuzi wao kwa ajili ya kuijenga nchi na kwamba manispaa imeona mbali katika kuwawezesha kwenye ufanisi huo ambao unatija kwa taifa.

SERIKALI imefungua mlango kwa mwekezaji anayetaka kuwekeza kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi