loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Inflantino kuchungwazwa tuhuma za rushwa

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo rushwa.

Mwendesha mashtaka wa nchini Uswisi, Stefan Keller alisema Alhamisi iliyopita alifungua uchunguzi wa jinai kwa Gianni baada ya kuona kuna dalili za mwenendo wa jinai katika mikutano kati yake na ofisa anayesimamia uchunguzi kuhusu ufisadi wa mpira wa miguu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za nchi ya Uswisi, Rais wa FIFA ni miongoni mwa viongozi wenye kinga, hivyo wanatakiwa kuombewa kuondolewa kinga ili wachunguzwe na tayari mwendesha mashtaka Mkuu wa Serikali ya Uswisi ameomba ruhusa kwa Infantino pamoja na mtuhumiwa mwingine ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Uswisi aliyejiuzulu Michael Lauber.

Uchunguzi wa tuhuma za rushwa ndani ya FIFA uliofanywa mwaka 2015 na kusababisha kumpa nafasi Gianni Infantino Februari 26, 2016 ya kuwa Rais wa FIFA, inaelezwa katika uchunguzi huo Infantino alitengeneza mazingira na kufanya uongo hivyo kunufaika kwa kuwa Rais wa FIFA.

Mwendesha mashtaka wa Zürich, Rinaldo Arnold ambaye ni rafiki wa utoto wa Infantino ambaye alimsaidia kupanga mikutano kati na wakili mkuu. Arnold pia yuko chini ya uchunguzi, ofisi ya Keller ilisema waendesha mashtaka walitaka kinga ya Lauber iondolewe ili aweze kuchunguzwa pia.

Katika taarifa yake, Keller alisema madai hayo katika malalamiko mapya mawili dhidi ya Infantino, Lauber na Arnold ni juu ya kutumia vibaya ofisi ya umma, uvujaji wa siri, kusaidia wahalifu na uchochezi kukiuka sheria.

Infantino amepuuza madai hayo kwani yamekuwa mwelekeo na shauku ya vyombo vya habari vya Uswisi na Ujerumani.

Katika taarifa yake ya Alhamisi iliyopita, Infantino aliahidi kuendelea kusaidia uchunguzi wa Uswisi katika FIFA.

"Watu wanakumbuka vizuri FIFA ilikuwa kama taasisi huko nyuma mwaka 2015, na jinsi gani uingiliaji wa mahakama ulihitajika kusaidia kurejesha uaminifu wa shirikikisho," Infantino alisema.

"Kama Rais wa FIFA lengo langu toka siku ya kwanza bado ni kusaidia mamlaka ya kuchunguza makosa ya zamani ya FIFA

KLABU ya Manchester United inamuwinda kwa ...

foto
Mwandishi: ZURICH, Uswisi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi