loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Moore kutimka Liverpool

OFISA Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Peter Moore, anatarajia kuachiwa wadhifa wake na nafasi yake itachukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji na Ofi sa Mkuu wa Kibiashara, Billy Hogan.

Mkataba wa miaka mitatu wa Moore unamalizika msimu huu wa joto na anarudi Marekani na mkewe, ambapo alifanya kazi kwa miaka 36 na makampuni ya Sega, Reebok, Microsoft and EA kabla ya kujiunga na klabu yake ya nyumbani mwaka 2017.

Atasimamia kipindi cha mpito hadi mwishoni mwa Agosti.

Hogan ambaye amewahi kufanya kazi na wamiliki wa Fenway Sports Group, tangu 2004 anaanza kama Mkurugenzi Mtendaji kuanzia Septemba,1. Hogan mzaliwa wa Marekani amesaidia kubadilisha utajiri wa kibiashara wa Liverpool chini ya FSG na kufanya mazungumzo kuhusu mpango mpya wa Nike ambao umeanza jana.

Mpango huo, ulikaa Mahakama Kuu baada ya mzozo wa kisheria na wauzaji wa zamani, New Balance unastahili dhamana ya pauni milioni 30 kwa mwaka kwa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu pamoja na mrahaba wa asilimia 20 kwenye mauzo ya jumla. Hogan alisema:

“Kwa kuwa nimepata bahati ya kufanya kazi katika klabu hii kwa zaidi ya miaka nane, ni heshima kubwa kuchukua jukumu la ofisa mtendaji mkuu na kuendelea na kazi kubwa ambayo imefanywa hivi sasa katika shirika lote.

“Ninamshukuru mmiliki mkuu, John Henry, mwenyekiti, Tom Werner, na Rais Mike Gordon, Rais wa FSG kwa nafasi hii ya kuongoza biashara katika hatua inayofuata ya sura ya kufurahisha”.

Jukumu la Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool lilibadilishwa baada ya kuondoka kwa Ian Ayre na Gordon, Mkurugenzi wa Michezo,Michael Edward, na Meneja, Jürgen Klopp, kushughulikia harakati za kila siku za uendeshaji wa mpira. Moore, shabiki wa Liverpool wa maisha yote, alisema:

“Nimeipenda kila dakika kazi ya hapa Liverpool na ninajiona nina bahati ya kuendelea mbele na shughuli za klabu, kibiashara na jamii katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

“Imekuwa safari ya kushangaza na nilipenda kulipa fadhila kwa John, Tom na Mike kwa kunipa nafasi ya kuongoza shughuli za biashara Liverpool.

“Kufikiria tumeshinda Ligi ya Mabingwa, Kombe la Uefa, Kombe la klabu la dunia la Fifa na sasa taji la Ligi Kuu wakati wangu ni njia zaidi ya ndoto zangu. Imekuwa mafanikio mazuri na meneja, wachezaji na wafanyakazi.

Timu inastahili kabisa malalamiko na kutambuliwa na kumbukumbu nitakazozithamini milele,” Aliongeza: “Nilirudi Liverpool mwaka 2017 nilikuwa nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 30 na imekuwa ni uzoefu maalum.

Mke wangu na mimi tulioana hapa miaka miwili iliyopita na tunarudi Marekani na hisia mchanganyiko,”.

“Amefurahi na tunatarajia kuunganishwa tena na familia zetu na watoto waliokua nchini Marekani, tukiwa na hisia za kuachana na Liverpool ambayo tumeipenda kila dakika na fursa ya kufanya mabadiliko na kuacha alama yetu katika historia ya mji huu mkubwa na klabu,”.

KLABU ya Manchester United inamuwinda kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi