loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara 141 wapewa vyeti, leseni za ubora za TBS

WAFANYABIASHARA 141 wakubwa, wa kati na wadogo nchini, wamekabidhiwa vyeti na leseni za kutumia alama ya ubora ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), baada ya bidhaa wanazozalisha kuthibitishwa kukidhi viwango vya ubora.

Kati ya wazalishaji hao, 58 ni wazalishaji wadogo wanaozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo vitakasa mikono, vyakula, vilainishi, vifaa vya umeme na vya ujenzi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kukabidhi leseni hizo kwa wazalishaji hao, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Yusuf Ngeya alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa shirika kuwakabidhi vyeti na leseni za kutumia alama ya ubora wazalishaji ambao wanakidhi vigezo ili waendelee na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora.

Alisema kuwa hatua ya bidhaa hizo kupatiwa vyeti na leseni za kutumia alama za ubora za shirika hilo, kutawafanya wazalishaji hao kuwa na uwezo wa kushindana na bidhaa nyingine sokoni, kuuza nchi za Afrika Mashariki bila bidhaa zao kulazimika kupimwa tena kwa ajili ya kuzithibitisha ubora na watapanua wigo wa biashara zao kwa kuyafikia masoko mengi zaidi.

“Ni wakati mwafaka wa kuwapongeza na kuwapa moyo wajasiriamali wadogo ili nao waweze kuwa wakubwa kama wengine, tunakabidhi vyeti na leseni za ubora kwa wajasiriamali na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu na hii ni kawaida yetu kila baada ya miezi mitatu kuwapongeza baada ya kupata vyeti vyao vya ubora na leseni,”alisema na Dk Ngenya na kuongeza: “Namshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fursa kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo bure pale wanapoomba bidhaa wanazozalisha wenyewe kuthibitishwa ubora na TBS” alisema.

Dk Ngeya aliwataka wajasiriamali hao kuwa mabalozi wazuri wa TBS, kwa kuhamasisha wananchi wanaojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenda kuthibitisha ubora wa bidhaa zao wanazozalisha. “Hakikisheni mnaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika kila siku na sio leo mnapata leseni na cheti, badala yake mnaanza kutengeneza bidhaa zisizokuwa na ubora, tutakuwa tunapita na kuwafanyia ukaguzi wa mara kwa mara kwani sheria inaturuhusu kufanya hivyo,”alisema. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ihnemeter inayozalisha na kuuza vifaa vya umeme ikiwemo mita, Abraham Rajakili, aliishukuru TBS kwa kuwapatia vyeti na leseni za ubora, kwani huo ni mwazo mzuri wa kuingia sokoni kwa kukubalika zaidi na kujiamini. “Kwa kweli tunawashukuru TBS kwa hatua hii, tunaamini kuwa bidhaa zetu zitaweza kufanya vizuri zaidi sokoni kutokana na kuwa na nembo za ubora za TBS,”alisema. Wakati huo huo, Dk, Ngenya alisema kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, TBS imesajili takribani majengo 513 ambayo yanashughulikia chakula na vipodozi na kusajili bidhaa ya chakula na vipodozi 596 kwa kipindi hicho. “Tangu mabadiliko ya sheria yafanyike na majukumu ya kusimamia sekta ya vyakula na vipodozi kuhamia kwetu (TBS),ni marufuku mfanyabiashara kuingiza chakula au vipodozi visivyosajiliwa sokoni na hata majengo yanayofanya shughuli hizi lazima nayo yaangaliwe ikiwemo migahawa, magari yanayobebea vyakula, maduka ya vyakula na vipodozi,”alisema. Kabla ya mabadiliko hayo, usimamizi wa chakula na vipodozi ulikuwa chini ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi