loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wananchi wahimizwa kujisajili RITA

WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umewataka wananchi kuchangamkia huduma zinazotolewa na wakala huo kwa manufaa yao ya sasa na ya baadaye.

Akizungumza katika viwanja vya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Nanenane mkoani Simiyu, Ofisa Habari wa RITA, Grace Kyasi alisema huduma zao zinagusa maisha ya kila mtanzania katika nyanja tofauti kama vile elimu, ajira, afya, mikopo ya elimu ya juu, ndoa, wosia na mirathi.

"Jamii yetu inahitaji kufahamu kuwa huduma za RITA ni huduma ambazo haziepukiki kwa maana ya kugusa maisha yetu ya kila siku katika jamii yetu, kwa mfano mtoto anapozaliwa atahitaji kupata cheti cha kuzaliwa, mtu anapofariki dunia ndugu watahitaji kufuatilia cheti cha kifo cha marehemu.

"Pia watu wanapofunga ndoa wanatakiwa kusajili vyeti vyao vya ndoa na vilevile tuna huduma ya kuandika na kuhifadhi wosia pamoja na usimamizi wa mirathi, " alisema.

Alitaja huduma nyingine zitolewazo na RITA ni usajili wa talaka, usajili wa bodi za wadhamini pamoja na kuasili watoto.

Alisema hata hivyo hivi karibuni wakala umeanzisha huduma ya usajili wa vizazi na vifo na uhakiki wa vyeti hivyo kwa njia ya mtandao, ambapo mtu anaweza kuipata huduma hiyo popote alipo nchini.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine