loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kabudi ataka Kanda ya Mashariki kusogeza mbele uchumi

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka mikoa iliyopo Kanda ya Mashariki kuhakikisha inatimiza majukumu yao katika uzalishaji wa mazao ili taifa liweze kusonga mbele kiuchumi.

Profesa Kabudi alisema hayo wakati akifungua maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane ) juzi katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro Alisema, mikoa inayounda kanda hiyo ambayo ni Morogoro, Tanga, Dar es Salaam na Pwani ina jukumu kubwa la kuzalisha mazao kwa wingi yatakayowezesha viwanda kupata malighafi za kutosha katika kukuza viwanda nchini.

Katika hatua nyingine Waziri huyo alitoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Morogoro kuepuka uharibifu wa mazingira kwa kuacha tabia ya kujenga juu ya milima na kulima kwenye vyanzo vya maji ili mkoa huo uweze kuwa na maji ya kutosha katika kuendeleza kilimo.

Naye Mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Paramagamba Kabudi , kufungua maonesho hayo ,alisema kwa sasa kanda ya Mashariki ipo tayari kwa maonesho ya kitaifa baada ya kupita miaka mingi kutokana na uzito wake .

Ndikilo , alisema unapoizungumzia Kanda ya Mashariki unazungumzia kilimo cha miwa ,mpunga ,mkonge , korosho na mazao ya mbogamboga pia ina bahari ya hindi kwa ajili ya uvuvi na mito mingi mikubwa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Maonesho ya wakulima , wafugaji na wavuvi mwaka huu 2020 yamebeba kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020.

SERIKALI imezindua Mpango Mkuu ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine