loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasimamizi wa uchaguzi fuateni sheria

UCHAGUZI Mkuu wa madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utafanyika Oktoba 28, mwaka huu. Kwanza tunaipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kueleza kuwa maandalizi ya shughuli hiyo yanaendelea vizuri na pia kwamba uchaguzi utakuwa huru, wa haki, unaoaminika na unaozingatia katiba ya nchi, sheria, kanuni na maelekezo ya NEC.

Pili tunapongeza tume hiyo kwa kuanza kuendesha mafunzo kwa waratibu wa mikoa, wasimamizi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa mikoa, wilaya na majimbo na vituo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa NEC, Dk Wilson Mahera, waratibu na wasimamizi hao wa uchaguzi wanatakiwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni na maelekezo ya tume na kamwe wasifanye kazi kwa mazoea.

Mahera anasema kuwa mafunzo kwa watu hao, yanawapa uzoefu na elimu ya jinsi ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka huu na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi.

Anataka waratibu na wasimamizi hao kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwemo viapo walivyoapa ili watende majukumu yao kwa mujibu wa sheria. Kama kila mmoja atatii kiapo alichoapa na kutunza siri, uchaguzi hautakuwa na changamoto zozote.

Vile vile wasimamizi na waratibu hao, wanatakiwa kujua na kutambua vyema maeneo wanayofanyia kazi, ikiwepo miundombinu ya kufika katika kata na vituo vya kupigia kura, ili kuwezesha upigaji kura kuanza mapema na kumalizika katika muda uliopangwa.

Watambue kuwa wameteuliwa kufanya kazi hiyo, kwa sababu wana uwezo wa kuwezesha uchaguzi huo kuwa mzuri na usiokuwa na malalamiko au vurugu.

Wanapotekeleza majukumu yao wanatakiwa kushirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa dini, hasa katika masuala ambayo wanastahili kushirikishwa.

Jambo lingine tunawahimiza wananchi waendelee kufanya maombi mara kwa mara kuombea uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili uwe wa amani na utulivu. Maombi ni kitu muhimu sana kwani kila anayeomba kwa moyo wa dhati, Mwenyezi Mungu hujibu kwa mambo mazuri.

GEITA ni mmoja wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi