loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Asilimia 45 ya walimu wajitokeza kugombea uongozi

WALIMU 91,000 ambao ni sawa na asilimia 45 ya walimu wote nchini walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

“Hii haijawahi kutokea lakini tunaona ni jinsi gani walimu wanapenda kuongoza wenzao na hii inaonesha kiasi gani wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kiasi gani sasa wanakijua chama.”

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wa CWT, Deus Seif wakati wa kongamano la Mwalimu Babalao lililoambatana na kuwaaga wahitimu wa mwaka wa tatu wa ualimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Alisema katika suala la CWT na wanachama wake, mwaka 2020 kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwa wanachama kukijua chama chao.

Alisema takwimu zinaonesha walimu waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali walimu zaidi ya 91,000 sawa na asilimia 45.

“Tanzania ina walimu 267,272 waliojitokeza ni zaidi ya 91,000 hii haijawahi kutokea, lakini pia tunaendelea kutekeleza maelekezo ya vikao mbalimbali kama vile kulipa mkono wa kwa heri kwa kutumia fedha kwenye akaunti za wahusika moja kwa moja,” alisema.

Alisema wanaendelea kwenye utetezi wa kesi mbalimbali, na kwa taarifa za mwisho iliyowasilishwa kwenye mkutano, CWT kupitia wanasheria wake imeshinda kesi kwa zaidi ya asilimia 98.

Katibu huyo alisema hadi kufikia Januari 2020, jumla ya walimu 106,367 kati ya walimu 267,272 wamepandishwa vyeo na kubadilishiwa mishahara yao, sawa na asilimia 40.1.

Alisema kuhusu malimbikizo ya mishahara kiasi cha Sh bilioni 38.8 kimelipwa kwa walimu 35,805 mpaka Juni 4, 2020.Madeni yasiyo na mshahara yaani likizo na uhamisho, jumla ya bilioni 358.1 zimelipwa kwa watumishi wakiwemo walimu hadi Juni 4, 2020, serikali itaendelea kulipa madeni hapo, pindi uhakiki ukikamilika, kwetu ni mafanikio.

Alisema Rais alishatoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuwa ahakikishe mwaka huu wa fedha walimu 166,548 wanaostahili kupandishwa vyeo wapandishwe.

“Benki yetu ya walimu tunaendelea kuiimarisha, wakati wa Mkutano mkuu Rais ameonesha kuridhishwa na ametuagiza kuendelea kurekebisha maeneo yaliyobakia,” alisema

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine