loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Prof Nyahongo ataka mjadala wa kitaifa walimu wanaosubiri

MKUU wa Ndaki ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Julius Nyahongo ameshauri kuitishwa kwa mjadala wa kitaifa ili kuona namna wanafunzi wa ualimu wanaotoka vyuo vikuu wanavyoweza kwenda kufundisha kwa kujitolea kwenye shule za kata wakati wakisubiri kupata ajira.

Alisema hayo juzi wakati wa kongamano la Mwalimu Babalao lililoambatana na kuwaaga wahitimu wa mwaka wa tatu . Kongamano hilo liliandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na Chama Cha Walimu wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma.

Profesa Nyahogo alisema shule za kata wakati wa kuanzishwa kwake mwanzoni zilibezwa sana na Watanzania ambao hawakuwa wazalendo.

Alisema wakati wa awamu ya nne kwenye uongozi wa Rais Jakaya Kikwete kilijengwa Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kilijibu maswali yote magumu ya kukosa walimu kwenye shule mbalimbali hususani za kata ambapo wanasiasa wengi walikuwa wakibeza.

“Tumezalisha walimu wengi sasa, miaka mitatu ijayo tutazalisha walimu 8,000 tumekidhi mahitaji ya taifa baada ya muda mfupi tutakuwa tumejaza soko,” alisema.

Alisema jambo la kujiuliza hao wanafunzi wakishahitimu wanakwenda wapi hilo swali linaweza kujibiwa kwa kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kupitia Wizara ya Elimu ili kuliweka kwenye mjadala wa kitaifa.

“Wanafunzi wanapohitimu wanaporudi kwenye vijiji vyao , tutengeneze utaratibu kila moja kwenda kwenye shule ya kata afundishe kwa kujitolea lakini hapo tunatakiwa kukaa na wizara mama na hata wakimpelekea Rais pendekezo letu atuelewe,” alisema.

Alisema ipo haja ya kuanzisha mfuko mahsusi kwa ajili ya walimu wanaomaliza vyuo warudi kwenye maeneo yao na hata ajira zitakapotoka walimu wenye nidhamu waajiriwe kwanza.

“Tusiwaache wakaelea hewani, wakiachwa wataona tasnia ya elimu haina maana, Ombi langu kwa CWT ambacho ni chama chenye nguvu, haya ni mawazo yangu binafsi tuchukue kama ni mjadala ambao ni wa kwetu sote,” alisema.

Katika risala yao wahitimu walitaja miongoni mwa mafanikio ya chama cha Walimu wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSTA) ni pamoja na kufanikiwa kuunda katiba itakayokuwa mwongozo wa utendaji wa shughuli zake.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine