loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

GGML,NEEC kujengea uwezo wafanyabiashara

KAMPUNI ya Uchimbaji wa Madini ya Geita (GGML) kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la Uchumi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), imesaini makubaliano ya utekelezaji wa programu maalumu ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara mkoani Geita kushiriki katika kushindania zabuni zinazotolewa na mgodi huo.

Makubaliano yaliyotiwa saini wiki iliyopita mkoani Geita, yatadumu hadi Juni 30, 2021.

Akizungumza katika hafla kusaini makubaliano hayo na kuzindua programu hiyo, Makamu Rais wa GGML, Simon Shayo alisema progamu hiyo inalenga kuwajengea uwezo wazabuni wa Geit kutambua na kuzingatia viwango na ubora wa bidhaa na huduma zinazohitajika kwa GGML.

Alisema programu hiyo inalenga kuunganisha wazabuni wa GGML na mamlaka za serikali, sekta binafsi na jamii zinazotoa fursa za kushiriki kikamilifu katika zabuni hizo.

“Programu hii itawawezesha wazabuni wa GGML kupata soko la uhakika la bidhaa na huduma wanazozalisha ili kujiongezea kipato cha mtu mmoja mmoja, cha kaya na jamii kuchangia pato la taifa la mtu mmoja,” alisema.

Alisema GGML itaweza kupata huduma na bidhaa zenye ubora kutoka kwa wazabuni wa ndani zitakazoongeza tija kwa wazalishaji hao.

“GGML tumejitolea katika maendeleo endelevu ya jamii. Tunapenda kuacha urithi, hata wakati madini yatakapokuwa yamechimbwa. Kusudi ni kuongeza ushiriki wa Watanzania shughuli za mgodi ili kusaidia jamii ambayo tunafanya nayo kazi.

Tunaonyesha haya Geita kwa kuwa washirika dhabiti na Serikali kuboresha huduma za jamii, elimu, afya na kilimo, “alisema Shayo. Shayo alisema GGML inajivunia kuwa walipa kodi bora na wakubwa nchini ambapo mwaka 2019, kodi iliyolipwa na GGML kwa serikali ilikuwa takriban Sh bilioni 467 sambamba na kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 5,000.

Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (sera, uratibu na uwekezaji), Dorothy Mwaluko alisema programu hiyo imekuja wakati mzuri.

“Itahakikisha changamoto za kampuni za Kitanzania kushindwa kupata zabuni kwenye uwekezaji nchini, zinatatuliwa na kumwezesha mwekezaji kutekeleza kikamilifu sheria za nchi kwa kununua bidhaa na kutumia huduma za Watanzania zinazokidhi viwango vya kimataifa.

“Niwapongeze Kampuni ya Uchimbaji Geita, GGML kwa kuwezesha programu hii kwa kuwa wafanyabiashara watakaonufaika na mafunzo haya mbali na kushiriki uzalishaji katika mgodi huu, yatawafungulia njia kushiriki katika miradi inayotekelezwa katika sekta nyingine,” alisema.

Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa alisema uzinduzi wa programu hiyo unabebwa na kauli mbiu ‘‘Ushiriki na Ushindani wa Uwazi katika Kukuza Uchumi’’. Alisema kauli mbiu hiyo inajielekeza kujenga uwezo kwa wafanyabiashara wa ndani wapate fursa ya kushiriki uendelezaji sekta ya madini.

SERIKALI imezindua Mpango Mkuu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine