loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri ateua mameneja Tanroads Lindi, Pwani

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amemteua Lucas Mlavi kuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Lindi na Dustan Sindano kuwa Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani.

Mlavi anachukua nafasi ya Issac Mwanawima aliyekuwa Meneja Mkoa wa Lindi na Sindano anachukua nafasi ya Yudas Msangi, aliyekuwa akikaimu nafasi ya Meneja Tanroads Mkoa wa Pwani.

Kamwelwe alitangaza uteuzi huo akiwa wilayani Mbarali, Mbeya akikagua barabara ya Mbeya/Iringa, inayoendelea kurekebishwa kutokana na kuharibika wakati wa mvua za mwaka huu.

Waziri huyo alitengua mameneja hao wawili siku moja baada ya Rais John Magufuli kupita kwenye barabara za mikoa hiyo akitoka Mtwara, kuhudhuria maziko ya Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Ubovu wa barabara hizo ulimkera Rais Magufuli. Kamwelwe aliwataka mameneja wa Tanroads, kutekeleza kwa wakati agizo alilotoa kwamba kila barabara iliyoharibiwa na mvua zilizonyesha ikarabatiwe kabla ya mwisho wa mwezi huu kwa kuwa serikali ilishatoa Sh bilioni 39 kupitia Mfuko wa Barabara kwa ajili ya kazi hiyo.

Alisema kuwa meneja yeyote atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo, atachukuliwa hatua kwa kuwa atakuwa ameshindwa kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Meneja yeyote atakayesumbua nitalala naye mbele. Fedha zilikwishatolewa kwa kila mkoa kulingana na mahitaji yake. Kilichobakia ni utekelezaji, sasa kwa nini tuendelee kuwa na watu wasiotekeleza maagizo wakati fedha zilikwishatolewa na serikali kwa ajili ya kuwaondolea adha wananchi”alisema Kamwelwe.

Aliagiza ndani ya siku saba ziwekwe alama za wavuka kwa miguu barabarani katika maeneo ya shule za msingi Mabadaga na Nyangulu na Shule ya Sekondari Malenga.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Habari Nyingine