loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bil 52/- zakusanywa mpakani Namanga miezi 6

KATIKA miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu Kituo cha Forodha cha Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya, kimekusanya zaidi ya Sh bilioni 52 sawa na asilimia 86 ya malengo.

Meneja wa kituo hicho, Poul Kamkulu aliyasema hayo hivi karibuni wakati akitoa taarifa ya kazi kwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Iddy Kimanta aliyetembelea kituo hicho kuangalia utendaji kazi na changamoto zinazowakabili watendaji mpakani hapo.

Kamkulu alisema lengo la makusanyo katika kituo hicho lilikuwa kukusanya Sh bilioni 54, lakini hawakufikia malengo kutoka na sababu ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid 19) iliyoathiri ukusanyaji mapato.

Alisema kuwa licha kuwepo Covid-19 wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha ikiwemo Sh milioni 125 za bidhaa zilizokamatwa kimagendo, zikipitishwa kwa kwa njia zisizo halali.

Kamkulu alisema kuwa kiwango kilichokusanywa ni mapato ya bidhaa zilizokuwa zikipelekwa nje ya nchi kupitia mpaka huo, zikiwemo bidhaa za kilimo, mifugo, madini na bidhaa za viwandani. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kimanta aliwapongeza watumishi wa forodha wa kituo cha Namanga, kwa kukaribia kufikia malengo na kuwataka kujituma zaidi.

SERIKALI imezindua Mpango Mkuu ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine