loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Warusi waongeza utafutaji taarifa kuhusu Tanzania

MASLAHI ya Urusi Tanzania yameongezeka baada ya Naibu Waziri Mkuu, Tatyana Golikova kuitaja kama moja ya nchi tatu za Afrika ambayo safari za ndege kutoka Urusi zitaanza kuanzia Agosti Mosi, mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yandex, tangu kutangazwa safari za ndani ya nchi hiyo, utafutwaji taarifa za Tanzania katika mtandao umeongezeka mara 65 zaidi ya kawaida.

“Tangu Julai 24, mwaka huu, shauku kuifahamu Tanzania katika mtandao wa Yandex ilipanda kuliko nchi yoyote,” ilisema taarifa ya Yandex. Watumiaji wa mtandao huo wa Yandex wengi walionekana kutaka kujua mahali ilipo Tanzania katika ramani, namna inavyoonekana, muda wa safari za ndege kwenda nchini humo, tathmini za watalii kuhusu nchi hiyo na hali ya hewa.

Ijumaawiki iliyopita Serikali ya Urusi ilitangaza kurejesha safari za ndege katika anga lake na kutaja nchi ambazo ndege za Urusi zitafanya safari ambazo mbali na Tanzania ni Uturuki na Uingereza kuanzia Agosti Mosi, mwaka huu.

Msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Maria Zakharova alisema kuwepo kwa Tanzania orodha ya nchi ambazo Urusi itafanya safari zake za ndege kunatokana na umaarufu wa nchi hiyo kwa watalii wengi wakirusi.

WAFUNGWA zaidi ya 200 ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi