loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RwandaAir yatua nchini, KLM nayo kutua leo  

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri wa ndege yamefungua rasmi safari zake na kuanza kutua nchini hususani katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Akizungumza mapema leo katika uwanja wa KIA baada ya kupokea ndege ya Shirika la Rwanda Airline, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendeshaji na Uendelezaji wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wa Kia (KADCO),Christine Mwakatobe  amesema tayari mashirika ya ndege manne yameshafanya safiri zake na kutua katika uwanja wa Kimataifa wa KIA.

Mwakatobe alisema Juni mosi mwaka huu walipokea ndege ya Ethiopia Airline, Julai 30-Qatar Airline, Agosti Mosi- Crystal na Agosti 4 yaani leo wamepokea Rwanda Air na pia wanatarajia kupokea ndege ya Shirika la ndege la KLM.

"Tumefurahi sana kwa shirika la ndege la Rwanda kuanzisha tena safari zake baada ya awali kusitisha kutokana na ugonjwa wa Covid-19," alisema Christine.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Rwanda, Jammy Mitali amesema shirika hilo limerudisha safari zake Tanzania, baada ya kuona hali ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 ipo shwari.

 

*Soma zaidi kesho kwenye Gazeti la Habari Leo...

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: John Mhala, KIA

Post your comments

Habari Nyingine