loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha aongezewa mkataba mkataba AS Kigali

ERIC Nshimiyimana amekubali mkataba mpya na sasa ataendelea kuwa Kocha Mkuu wa AS Kigali hadi mwaka 2022, klabu hiyo imetangaza mwishoni mwa wiki.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Rwanda amepewa jukumu la kuiongoza timu hiyo yenye maskani yake Nyamirambo angalau kutwaa taji moja kubwa katika kipindi chake hicho cha miaka miwili. Klabu hiyo imesema:

“Tumeamua kumuongezea miaka mingine miwili, kwani ni mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa zaidi nchini. Tumemtaka kushinda angalau taji moja kubwa katika kipindi hicho.”

Nshimiyimana, 48, atafanya kazi pamoja na Djabir Mutarambirwa kama kocha msaidizi, akichukua nafasi ya Jean de Dieu Mateso ambaye mkataba wake haukuongezwa.

Mutarambirwa anaungana na klabu hiyo inayodhaminiwa na Jiji la Kigali baada ya kutupiwa virago kama kocha msaidizi wa SC Kiyovu miezi miwili iliyopita.

AS Kigali ilimaliza katika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya Rwanda ya 2019/20, ambayo ilimalizika mapema tangu Mei kutokana na mlipuko wa janga la Covid-19.

Wakati huohuo, kocha wa makipa Thomas Higiro naye pia ameongeza makataba wa miaka miwili katika klabu hiyo ya AS Kigali hadi mwishoni mwa msimu wa mwaka 2021/22.

KOCHA wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema ndoto yake ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi