loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kipa Gor asikitika Singida kushuka

KIPA wa Gor Mahia, David Mapigano ameeleza kusikitishwa kwake baada ya timu yake ya zamani ya Singida United kushushwa daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kipa huyo Mtanzania alijiunga na K’Ogalo katikati ya mwaka jana akitokea Singida United kwa mkataba wa miaka mitatu na kumpiga bao kipa mkongwe Boniface Oluoch aliyekuwa chaguo la kwanza katika timu hiyo.

SINGIDA KUSHINDWA:

Mapigano anasema kushindwa kwa Singida kusa jili wachezaji wazuri wapya wakati wa dirisha lililopita la usajili ndio sababu kubwa ya timu hiyo kushuka daraja.

“Ni huzuni kwa timu iliyonikuza kushuka daraja hadi la Kwanza. Tatizo kubwa ni kushindwa kusajili wachezaji wazuri wapya baada ya kuondokewa na wengine iliyowategemea, nina matumaini watapambana na kupanda tena,” alisema Mapigano kutoka Arusha.

Singida ilimaliza katika nafasi ya mwisho kati ya timu 20 baada ya kushinda mechi nne tu msimu mzima, huku Lipuli na Ndanda nazo zikiwa zimeshuka wakati Simba ikitwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo ikiwazidi Yanga kwa pointi 18.

KOCHA wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema ndoto yake ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi