loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vipimo waanza kutoa elimu ya ufungashaji

WAKALA wa Vipimo (WMA) imeanza kutoa mafunzo sahihi kwa wajasiriamali ya kufungasha bidhaa kwa kutumia vipimo sahihi na kuandika alama kwa usahihi katika kifungashio kwa lengo la kuongeza thamani za bidhaa wanazozalisha.

Akizungumza na HabariLEO katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu kwenye Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi jana, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Wakala wa Vipimo, Deogratias Maneno alisema mafunzo hayo wanatoa kwa wajasiriamali na wananchi wengine wanaotembelea banda la wakala huo.

Alisema kwa kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa wakulima bado wanaendelea kuuza pamba katika vituo mbalimbali vilivyothibitishwa, wakala huo inatoa elimu ya utambuzi wa mizani sahihi iliyohakikiwa kwa kutumia mifano ya mizani iliyoidhinishwa kununulia zao hilo.

Mizani sahihi iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo na kupitishwa kwa matumizi hufungwa lakiri ambayo huonesha alama ya ngao ya taifa na tarakimu mbili za mwisho za mwaka husika mfano “20” ikiwakilisha mwaka 2020.

Pia mizani iliyohakikiwa huwekewa stika maalumu ya Wakala wa Vipimo. Maneno alisema upande wa suala la uharibifu wa mizani katika ununuzi wa pamba umepungua sana katika siku za hivi karibuni ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Moja ya sababu zilizochangia kushuka kwa matukio hayo ni kuimarishwa kwa utendaji wa ushirika, ambapo ununuzi hufanyika,” alisema.

Aidha, katika maonesho hayo alisema, Wakala wa Vipimo inaonesha namna ya utambuzi wa mizani sahihi iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo inayotumika katika ununuzi wa vito na madini.

Hilo linakwenda sambamba katika kufanikisha jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhakikisha wananchi wake wanafaidika na vito na madini yanayopatikana hapa nchini.

Maneno aliwataka wafanyabiashara kufanya kazi zao kwa uadilifu na kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo sura namba 340 na mapitio yake, endapo mtu yeyote atabainika kutenda kosa kinyume na Sheria hiyo na akakiri kutenda kosa husika, atapaswa kulipa faini isiyopungua Sh 100,000 na isiyozidi Sh milioni 20 kwa kosa la kwanza, endapo mtuhumiwa atakataa kukiri kosa na kufikishwa Mahakamani kwa kosa hilo, na akabainika kutenda kosa hilo, atatozwa faini isiyopungua Sh 300,000 na isiyozidi Sh milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.

Aidha, endapo mtuhumiwa atakamatwa na kosa kwa mara ya pili na kuendelea na akipelekwa Mahakamani akakutwa na hatia, adhabu ni faini isiyopungua Sh 500,000 na isiyozidi Sh milioni 100 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Maonesho ya NaneNane 2020 Na Lucy Ngowi, Bariadi MBEGU za mpunga zinazotokana na maboresho ya mbegu za kienyeji, ikiwamo supa zimezalishwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na upungufu wa mvua.

Meneja kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Ifakara Morogoro, Dk Atugonza Bilaro alisema hayo katika viwanja vya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Nanenane vilivyopo Nyakabindi mkoani wa Simiyu.

Alisema mbegu hizo pia zina tija kwa wakulima wale ambao wanahitaji kulima misimu zaidi ya mmoja kwa mwaka, kwani zinatoa mavuno mengi hadi mara tatu ya mbegu za kienyeji.

Dk Bilaro alitoa mfano kwa kusema mbegu aina ya TARI RIC1 imetengenezwa mahsusi kuwa mbadala wa aina ya mbegu ya supa kwa kuwa ina mavuno mara mbili zaidi.

Pia alisema aina ya TARI RIC2 imetengenezwa mahsusi kwa kilimo cha kutegemea mvua pia inakomaa mapema kiasi cha kuwezesha wakulima wenye maeneo ya umwagiiaji kulima mara mbili au zaidi kwa mwaka.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo ya utafiti ina mbegu za mpunga zinazofaa kulimwa maeneo yasiyotuamisha maji aina ya NERICA na zile zinazovumilia kwenye maeneo ya chumvi chumvi ambazo ni SATO1 na SATO9.

“Mbegu zote hizi zinapatikana TARI Ifakara na Dakawa,” alisema.

Alisema mavuno ya mbegu hizo ni wastani wa tani sita hadi nane kwa hekta tofauti na mbegu za kienyeji ambazo huzaa wastani wa tani 0.5 hadi 1.5

BIASHARA ya masoko ya madini inazidi kupaa na kuwezesha wajasiriamali ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi