loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Deni la taifa sasa kufikia trilioni 5.6/

DENI la taifa la Kenya linatarajiwa kuongezeka hadi kufi kia Sh trilioni 5.6 za nchi hiyo hadi kufi kia Juni, mwakani.

Kwa mujibu wa ripoti ya deni la taifa iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni, mpaka kufikia mwaka 2022 ambao ni mwaka wa kuondoka madarakani kwa Rais Uhuru Kenyatta, deni la taifa linatarajiwa kupanda hadi kufikia Sh trilioni 7 za nchi hiyo.

Taarifa ya Wizara ya Fedha ambayo iliwasilishwa bungeni ilisema mpaka kufikia Juni, mwaka huu, deni la taifa lilikuwa Sh trilioni 5.1 za Kenya, ambapo kati ya hizo Sh trilioni 2.5 lilikuwa ni deni la ndani na Sh trilioni 2.6 deni la nje.

Katika deni la nje, ripoti hiyo imeonesha kuwa, mchangiaji mkubwa wa deni hilo ni China ambayo imekuwa mstari wa mbele kukopesha katika miradi mbalimbali ya nchi hiyo.

China inaongoza kwa kutunisha deni la nje kwa Sh bilioni 559.1, ikifuatiwa na Italia ambayo inadai Sh bilioni 101.9, Ujerumani inashika nafasi ya tatu ikidai Sh bilioni 34.7.

Mataifa mengine yanayoidai Kenya na kuimarisha deni la nje ni Ubelgiji Sh bilioni 10.2 na Marekani inayodai Sh bilioni 2.9 za Kenya.

Mbali na nchi hizo, pia deni la nje limechangiwa na taasisi za nje kama vile Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) Sh bilioni 516.8, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Sh bilioni 204.8 na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) Sh bilioni 71.6.

JUMUIYA ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacifi c (OACPS) ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi