loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jumuiya za CCM zahimiza kura nyingi za ndio kwa Magufuli

JUMUIYA zote za Chama cha Mapinduzi (CCM), zimetakiwa kushirikiana kuhakikisha mkoa wa Dodoma unalinda historia yake ya kuongoza kwa kupata kura nyingi za Urais kama ilivyokuwa mwaka 2015.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga wakati akizungumza katika kikao cha baraza la Jumuiya ya Wazazi la CCM mkoa lililokuwa maalumu kwa ajili ya kumchagua mwakilishi wa jumuiya hiyo katika nafasi ya ubunge.

Mbanga alisema ili hilo lifanikiwe ni muhimu kuhamasisha watu kujitokeza kupiga kura kwa wingi. “Mwaka 2015 Dodoma ilishika namba moja kwa kumpa kura nyingi Rais John Magufuli, sasa lazima tujipange tuhamasishe wanachama wetu wakapige kura ili tupate kura za kishindo kwa Rais hata kwa madiwani na wabunge,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma, Damas Mukasa alisema kama lilivyo jukumu la jumuiya hiyo kulea basi watashirikiana na jumuiya zote kuhakikisha lengo la kushinda uchaguzi linafanikiwa.

Katika uchaguzi huo, Egla Mwamoto aliibuka mshindi kwa kura 36 kati ya kura 39 zilizopigwa huku mgombea mwenzake Erna Hallo akipata kura tatu.

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Kondoa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi