loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uchumi Tanzania upo vizuri

VITA dhidi ya rushwa, ufi sadi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotoa ajira kwa maelfu ya Watanzania, ni moja ya mambo yanayopingana na kilichoelezwa kwenye makala ya jarida la The Economist kwamba uchumi wa Tanzania ni mbaya.

Mafanikio mengine ni utoaji wa huduma na mikopo na faida katika taasisi za fedha na kampuni za uwekezaji nchini.

Ripoti za mashirika makubwa ya dunia, ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zimethibitisha kuwa pamoja na changamoto kadhaa, Tanzania inafanya vizuri kiuchumi na Julai Mosi mwaka huu Benki ya Dunia iliitangaza kuwa nchi ya uchumi wa kipato cha kati.

Mwasisi wa mtandao wa Global Value Hunter. com na African Lions Fund, Tim Staermose ameeleza kwa kina mafanikio ya kiuchumi yaliyofikiwa na Tanzania kwa kuangalia maeneo kadhaa ukiwemo uwekezaji, ukuaji wa faida na utoaji wa mikopo kwa benki nchini ikiwa ni ishara ya wazi kuwa ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia saba kufikia mwisho wa mwaka jana ni sahihi.

Staermose katika mtandao wake aliieleza kuwa taarifa ya The Economist ya Julai 23 mwaka huu kuwa uchumi wa Tanzania ni mbaya, siyo ya kweli na ni ajenda iliyojificha, inayotaka kudhoofisha uongozi mahiri wa Rais John Magufuli, lakini lengo hilo halitafanikiwa.

Alisema Rais Magufuli amethubutu kufanya mambo makubwa, yanaopaisha uchumi wa Tanzania na kusisitiza kuwa makala hiyo ni ya uongo na ya kupikwa, yenye nia mbaya kwa Tanzania, hasa wakati huu nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Akitoa mifano katika taasisi za fedha, kujibu makala hiyo kuwa benki hazitoi mikopo kwa kampuni zinazowekeza kwa sababu hazipati faida kutokana na uchumi mbovu, Staermon alisema benki kubwa mbili nchini Tanzania za NMB na CRDB ambazo zinachukua asilimia 40 ya sekta ya benki nchini, zote ziliripoti ukuaji mkubwa wa mikopo kwa mwaka jana 2019.

Kwa mfano, ripoti ya kila mwaka ya NMB ilionesha kuwa mwaka hadi mwaka mikopo na maendeleo kuna ukuaji mzuri wa asilimia 11 hadi Sh bilioni 3,596 mwaka jana kutoka Sh bilioni 3,252 mwaka 2018.

Kwa upande wa CRDB, malengo yao ya kusaidia biashara na watu binafsi kupitia mikopo, yamepanda kwa asilimia nane hadi Sh bilioni 3,382.0 mwaka jana, ikilinganishwa na Sh 3,126.7 bilioni zilizoripotiwa mwaka 2018.

CRDB katika ripoti yake ya kila mwaka ya mwaka 2019 ilieleza kuwa ukuaji huo ulichochewa na juhudi endelevu za benki kuinua biashara ndogo na za kati (SME) na sekta za watumiaji.

“Sijui The Economist kupitia makala isiyo na jina la mwandishi, ni wapi wametoa takwimu hizo lakini data za msingi zinadhihirisha wazi kuwa benki za Tanzania zipo katika hali yenye afya zikitenga mikopo zaidi kwa sekta binafsi kwa mwaka 2019 zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2018,” alisema Staermose.

Alisema kuwa hali ya ufanisi mzuri wa benki umeendelea vizuri kwa mwaka huu wa 2020. Alitoa mfano wa NMB kuwa eneo la mikopo na maendeleo lilikua kwa asilimia 3.1 kutoka Januari 1 hadi Machi 31 mwaka huu na kwa asilimia 2.7 kutoka Aprili 1 hadi Juni 30, mwaka huu.

“Ukiweka kwa mwaka utaona kwamba ukuaji wa mkopo utakuwa wa tarakimu mbili pia kwa mwaka huu 2020,” ameeleza Staermose.

Alibainisha kuwa ukuaji huo kwa benki ya CRDB, ni imara zaidi kwa asilimia 3.1 katika robo ya kwanza ya mwaka 2020 na asilimia 3.8 kwa robo ya pili, ikiwa ni tafsiri ya ukuaji wa tarakimu mbili kwa mwaka ambayo ni zaidi ya asilimia 12.

Kwa upande wa mapato kwa kila hisa, NMB ilifikia Sh 187 kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza kwa mwaka huu 2020 na mwaka mmoja uliopita ilikuwa Sh 113 huku CRDB ikiwa na Sh 27 kwa nusu mwaka ya kwanza ya 2020 ikilinganishwa na Sh 23 ya miezi sita ya kwanza kwa mwaka 2019.

Kwa upande wa saruji, kwa mwaka 2019 Kampuni ya Twiga iliuza asilimia sita zaidi ya saruji kwa kiwango zaidi ya ilivyokuwa kwa mwaka 2018 na katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu 2020, Twiga tayari imeuza asilimia nane zaidi ya saruji zaidi ya ilivyouza kipindi hicho mwaka 2018.

Alisema hakuna ukweli kwamba kampuni za saruji hazifanyi vizuri katika uzalishaji nchini Tanzania, kwa kuwa kila mwenye macho anaona namna kwa mfano saruji ya Twiga inavyotumika kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), barabara, madaraja ya juu na ya kawaida, upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere.

Alisema kuwa taarifa kwamba mauzo ya bia kwa kampuni za bia ikiwemo TBL yalishuka kwa asilimia tano mwaka 2019 siyo ya kweli. Alisema kuwa ukweli upo katika ripoti ya mwaka ya TBL iliyofafanua kwa kina sababu za hali hiyo iliyochangiwa pia na udhibiti wa matumizi ya mifuko ya plastiki na pia vifungashio vya bia vilivyokosa vigezo. Lakini, hata hivyo faida iliongezeka kwa TBL mwaka jana.

“Kwa mara nyingine tena, mafanikio haya kwa takwimu ni uhalisia wa wazi wa uchumi ulioripotiwa kukua kwa takribani asilimia saba kwa mwaka,” alisema Staermose. Rais Paul Kagame

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi