loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mlipuko waua 100, wajeruhi 4,000

WAOKOAJI nchini Lebanon wanatafuta zaidi ya watu 100 waliokufa na 4,000 waliojeruhiwa kutokana na mlipuko mkubwa, ulioikumba bandari ya Beirut juzi.

Mji wote ulitikiswa na mlipuko huo, ulioanza kwa moto katika bandari na kusababisha kutokea moshi mweusi. Rais Michel Aoun alisema kuwa tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.

Aliitisha kikao cha dharura jana na kutangaza hali ya dharura kwa muda wa wiki mbili . Pia Rais alitangaza kwamba serikali itatoa dola za Marekani milioni 66 kutoka Hazina kwa ajili ya dharura.

“Tunachokishuhudia ni janga kubwa’’, alisema Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu, George Kettani alipozungumza na vyombo vya habari. Aliongeza kuwa wameshuhudia waathirika wa mlipuko huo kila kona ya jiji hilo.

Uchunguzi wa chanzo cha mlipuko huo unaendelea Baraza Kuu la Ulinzi nchini Lebanon lilisema wale watakaobanika kwa namna moja au nyingine kuhusika na mlipuko huo, wataadhibiwa vilivyo.

Ammonium Nitrate ilikuwa imeshushwa kutoka kwenye meli iliyokamatwa katika bandari hiyo mwaka 2013 na kuwekwa katika ghala.

Mlipuko huo umetokea wakati taifa hilo lipo katika mgogoro wa kiuchumi, unaosababishwa na mgawanyiko wa jadi. Pia taifa linakabiliwa na ugonjwa na virusi vya corona.

Vyombo vya habari vilionesha watu wakiwa wamenasa chini ya vifusi.

Shahidi mmoja alidai kuwa mlipuko huo ulikuwa mkubwa, hali inayoweza kusababisha watu kuwa viziwi. Kanda za video zilionesha magari na nyumba zilizoharibika.

WAFUNGWA zaidi ya 200 ...

foto
Mwandishi: BEIRUT, Lebanon

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi