loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwanafunzi abuni gari shamba la bei nafuu

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Musa Doto amebuni na kutengeneza hatua ya awali ya gari shamba litakalokuwa na uwezo wa kufanya kazi nane tofauti zinazohusu kilimo kwa ajili ya matumizi ya kumpatia unafuu mkulima mdogo nchini.

Doto, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa uhandisi, umwagiliaji na rasilimali maji wa chuo hicho amebuni gari hilo akiwalenga wakulima wadogo ambao hawana kipato kikubwa cha kununua matreta yanayouzwa kati ya Sh milioni 30 hadi 40.

Mwanafunzi huyo alisema hayo alipozugumza na HabariLEO jana kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Nane Nane Kanda ya Mashariki kwenye bandala la Shirika la Wajasiriamali Wahitimu wa kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUGECO) kuhusu ubunifu wa kutengeneza gari shamba.

“Mkulima mdogo hawezi kumudu kununua trekta… na gari shamba hili gharama zake ni gharama kubwa za kununua trekta na pia gari shamba hili linafanya kazi nyingi zinazomuhusu mkulima mdogo akiwa shambani,” alisema Doto kuongeza:

“Mashine hii kwa maana ya gari shamba hili inafanya kazi kuu nane zenye kumlenga moja kwa moja mkulima mdogo kwenye kazi zake sham bani , na vipuri vyake pia vitatengenezwa na mnunuzi anapewa muda wa uangalizi”.

Alitaja kazi nane kupitia gari shamba hilo mbali na usafiri wa shambani, nyingine ni kubeba mazao kutoka au kwenda shambani. Pia ni kituo cha pampu ya maji, kusukuma maji mpaka umbali wa mita 200, kuendesha kinu cha kupukuchua mahindi magunia 50 kwa saa moja.

Pia, alisema gari shamba hilo linaendesha kifaa cha kupulizia dawa shambani , inaendesha kifaa cha kupandia mazao mistari minne, kuweka mbolea shambani kwa mfumo wa kitaalamu na kufyeka majani na vyote hivyo katika mashine moja.

Hata hivyo, alisema licha ya ubunifu wa kutengeneza gari shamba hilo, bado anakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha hasa ikizingatiwa bado ni mwanafuzi, hivyo anahitaji kuwapata wadau wa kufanya nao kazi ya kukamilisha gari hilo ili liweze kutumika kikamilifu kwa wakulima.

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi