loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sh trilioni 3.463 zatumika kujenga barabara mitaani

KATIKA kipindi cha miaka mitano, serikali imetumia takribani Sh trilioni 3.463 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya barabara katika mamlaka za serikali za mitaa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo wakati wa kuelezea mafanikio katika sekta ya miundombinu na majengo ikiwa ni siku ya tatu ya maadhimisho ya Siku ya Tamisemi.

Alisema fedha hizo zikiwamo Sh trilioni 1.03 zilizoelekezwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ajili ya kutekeleza kazi zake na Sh trilioni 1.98 ambazo ni fedha maalumu zilizotumika kujenga mtandao wa barabara za lami katika miji ya kimkakati, manispaa na halmashauri za miji na jiji la Dar es Salaam.

Alisema hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa mtandao wa barara za lami kwa mamlaka ya serikali za mitaa kwa urefu wa kilometa 699.5 ambayo ni asilimia 52 kutoka kilometa 1,325.49 mwaka 2015 hadi kufikia kilometa 2,024.99 mwaka 2020.

Alisema kwa upande wa barabara za changarawe kulikuwa na barabara zenye urefu wa kilometa 22,089 na baada ya maboresho zimefikia urefu wa kilometa 24,193 ikiwa na ongezeko kwa asilimia 11 huku serikali ikiimarisha barabara za udongo na kufikia urefu wa kilometa 82,428 wakati madaraja makubwa yaliyojengwa ni 99.

Mtandao wa barabara zenye hali nzuri na wastani umeongezeka kutoka kilometa 61,798.45 hadi kufikia kilometa 63,164.74 sawa na ongezeko la barabara zenye hali nzuri na wastani urefu wa kilometa 1,366.29, hii inafanya barabara zenye hali nzuri kutoka asilimia 56 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 58 mwaka huu,alisema.

Jafo alisema mbali na barabara, lakini pia serikali imewezesha ujenzi wa stendi za kisasa 24, stendi za malori, masoko ya kisasa za mamlaka ya serikali, madapo ya kisasa katika baadhi ya miji.

Kuhusu  mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka katika Jiji la Dar es Salaam (DART), Jafo alisema ikiwa kazi za awamu ya pili ya mradi huo ikishika kasi, awamu ya kwanza imekuwa na mafanikio ya kuongeza abiria kutoka watu 75,000 kwa siku hadi kufikia abiria zaidi ya 200,000 kwa siku.

Bado tunaendelea na maandalizi ya kumtafuta mtoa huduma wa kudumu atakayekuwa na uwezo kutoa huduma ya mabasi 305 ikilinganishwa na mtoa huduma wa sasa ambaye ana uwezo wa kutoa huduma ya mabasi 140,alisema.

Naye Meneja wa Mfuko wa Barabara,  Eliud Nyauhenga alisema magari kuzidisha mzigo ni moja ya changamoto inayorudisha nyuma juhudi za serikali katika maendeleo ya sekta ya barabara.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi