loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EPZA yashauri wawekezaji kutumia fursa za Nanenane

MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji na Mauzo nje ya Nchi (EPZA) imewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa ya uwepo wa malighali nyingi za kilimo kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao, ili kuongeza thamani na kuweza kupata bei kubwa katika soko.

Hadi sasa kuna viwanda zaidi ya 170 ambavyo vimeanzishwa chini ya EZPA nchini na zaidi ya asilimia 40 ya viwanda hivi ni vile vilivyojikita katika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu, Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA, Grace Lemunge alisema kuongeza uwekezaji katika viwanda vya uchakataji mazao inaongeza thamani ya mazao na kumhakikishia mkulima soko la uhakika na ongezeko la kipato.

EPZA inatumia maonesho ya Nanenane ya mwaka huu kuwahimiza wawekezaji kutumia fursa kubwa iliyopo katika kilimo kuanzisha viwanda vya uchakataji mazao, jambo ambalo litapunguza uuzaji wa mazao ghafi nje ya nchi. Pia italiongezea taifa fedha za kigeni na kuongeza ajira zaidi,alisema.

Alisema mwekezaji katika maeneo maalumu ya uwekezaji ya EPZ na SEZ anafaidika na motisha maalumu inayotolewa na mamlaka pamoja na kurudisha upesi mtaji aliowekeza.

Sekta ya kilimo inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya watu na huchangia takribani asilimia 30 ya pato la taifa, hivyo uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao inamhakikisha mkulima soko la uhakika na hivyo kuweza kuongeza uzalishaji.

Ushiriki wetu katika maonesho ya Nanenane ni muhimu sana kwa sababu kilimo ndio ambacho hutupatia chakula na zaidi pia chanzo kikuu cha kipato cha familia nyingi,alisema.

EPZA inafanya kazi kwa karibu na viwanda vya kuchakata mazao kama vile dengu, mbaazi na choroko yenye soko kubwa India na nchi nyingine za Asia. Mamlaka huwaunganisha wakulima na viwanda hivi na kuweza kupata soko la uhakika.

Alisema hapo awali mazao haya yalikuwa yanatumika kwa ajili ya chakula pekee hapa nchini lakini sasa hivi imekuwa chanzo kikubwa cha kipato kwa wakulima.

Hivi karibuni serikali imeanza ujenzi wa kituo kikubwa cha biashara cha Kurasini ili kuweza kuibadilisha na kuifanya sekta ya kilimo kuwa ya kibiashara.

Mradi huu wa ujenzi wa kituo hiki ambacho kinatarajiwa kuwa kikubwa hapa nchini na katika eneo lote la ukanda wa Afrika Mashariki unatekelezwa na EPZA kwa thamani ya zaidi ya Sh bilioni 60.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi