loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wajasiriamali waliopata mafunzo Sido wanufaika

WAJASIRIAMALI wakubwa na wa kati waliopatiwa mafunzo na Shirika  la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ya kuzalisha bidhaa bora na zenye tija, wameanzisha viwanda huku baadhi yao kupata masoko ndani na nje ya nchi.

Kadhalika mafunzo hayo waliyopatiwa na shirika hilo wameonesha teknolojia mbalimbali, ubunifu wa bidhaa  wanazozalisha katika kipindi hiki cha serikali ya viwanda hapa nchini ambapo pia wataongeza pato la taifa.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini hapa, Ofisa Uendelezaji wa Biashara na Mafuzo (SIDO) mkoani Arusha, Bahati Mkopi alisema kuwa zaidi ya wajasiriamali 70 wameshiriki licha ya kuonesha ubunifu pamoja vifaa mbalimbali vyenye tija na ubora.

"Sido tunashirikiana  na taasisi zisizo za kiserikali, azaki halmashauri zote zilizopo mkoani hapa kuhakikisha kuwa tunapeleka teknolojia, mafunzo mbalimbali lengo likiwa ni kuzalisha bidhaa bora zenye tija ambazo zitauzwa kwa gharama nafuu ndani na nje ya nchi,"alisema.

Kwa upande wake mmoja wa wajasiriamali aliyewezeshwa na Sido na kunufaika na elimu hiyo kutoka Taasisi ya Sygita Product, Shyrose Gitasa ambaye ni mzalishaji wa bidhaa mbalimbali amewaomba watanzania kupenda kununua bidhaa kutoka nje ya nchi, ilihali hapa nchini vipo vingi vizuri na vinauzwa kwa gharama nafuu.

"Kutokana na uchumi kuyumba mjasiriamali si mimi pekee kwani tupo wengi kwa mfano mimi natengeneza masala aina zote, pilipili, na bidhaa zinginezo, ila kumuelewesha mteja hadi akuelewe utakua unatumia muda mwingi kwani wanapenda bidhaa zinazotoka nje ya nchi sijui ni kwa nini wateja hazikubali za kwetu," alisisitiza Gitasa.

 

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi