loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TARI yaalika wakulima kujifunza mbegu bora

WAKULIMA pamoja na wadau wameshauriwa kutembelea shamba la mazao mbalimbali ambalo limepandwa kwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti, pamoja na teknolojia za kisasa lililopo katika Viwanja vya Maonyesho ya Wakulima maarufu Nanenane vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI),  Eveline Lukonde alitoa ushauri huo katika maonesho hayo ambapo alisema teknolojia hizo zitakuwepo katika viwanja hivyo wakati wote.

Alisema kwenye shamba hilo watafiti mbalimbali wanaeleza jinsi teknolojia bora zinatumika ili kuhakikisha kilimo nchini kinakuwa cha faida na sio cha hasara.

"Kilimo cha tija, kuongeza mazao na uvunaji, kuhakikisha kwamba mkulima anaweza kukabiliana na magonjwa na wadudu waharibifu, pia kuhakikisha kwamba tunaongeza thamani hata kwenye yale mazao ambayo tunayagundua au mkulima anayatumia," alisema.

Alisema lengo ni teknolojia zimfikie mkulima huko alipo ambaye taasisi hiyo inafanya kazi kwa ajili yake, ikiwa ni pamoja na kuongeza kipato cha nchi.

"Serikali inaongeza kipato kwa sababu mazao mengine yanauzwa nje ambayo yanaingiza kipato kwa upande wa nchi pia kuweza kuingiza vitu mbalimbali," alisema.

Dk Lukonge alisema taasisi hiyo ina teknolojia ambazo zimefanyiwa utafiti kumsaidia mkulima kutokana na mabadiliko ya tabia nchini kwani wakati mwingine mvua inaanza kipindi ambacho si chake au kunyesha kidogo.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi