loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewataka Watanzania kutambua umuhimu wa mifumo ya fedha iliyoanzishwa na serikali kwa lengo la kupunguza vitendo vya rushwa na kuweka mazingira mazuri ya utawala bora.

Bashungwa alisema hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane kitaifa yanayoendelea katika vViwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu.

Alisema rushwa itapungua endapo kiwango cha kukutana kati ya mtu na mtu kitapunguzwa hasa katika masuala yanayohusu fedha.

"Mifumo ya fedha inayofanya kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ni ya kielektroniki, hivyo mtu anaweza kufanya malipo kwa njia ya simu ya mkononi katika ofisi yoyote ya serikali bila kukutana na mtu, na hatua hii itapunguza mazingira ya ushawishi wa rushwa," alisema Bashungwa.

Aliipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuweka sera nzuri za fedha ambazo zimesaidia kuifikisha nchi katika uchumi wa kati miaka mitano kabla ya wakati uliotarajiwa mwaka 2025.

Alisema Wizara anayoiongoza itaishirikisha Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kuelimisha wafanyabiashara wadogo na wenye viwanda kuhusu elimu ya biashara na utunzaji wa hesabu kuimarisha ujenzi wa uchumi wa viwanda.  

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alishauri suala la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika vifungashio vya mazaoya ndani ikiwemo pamba, korosho na kahawa liangaliwe upya ili kujenga ushindani dhidi ya mazao kutoka nje ambayo yamesemehewa kodi hiyo.

Akieleza kuhusu biashara ya mazao ya kilimo wakati wa changamoto ya ugonjwa wa Covid 19, Hasunga alisema baadhi ya nchi zimechukua hatua ya kufunga mipaka na kuzuia mizigo na wasafirishaji kuingia katika nchi hizo.

"Sisi kama Wizara ya Kilimo pamoja na wadau wengine, tumeathirika kwa kiwango kikubwa, tunakusudia kuwa na kikao cha pamoja katika Maonesho haya ya Nanenane kati ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara Pamoja na taasisi zake ili tuzungumze namna tutakavyokabiliana na changamoto zilizotokana na ugonjwa huo," alisema.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi