loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Tusiwageuze watunza misitu kuwa maharamia wa misitu’

WIKI iliyopita tulisikia namna baadhi ya viongozi wanavyozungumzia hatua ya serikali kuja na kanuni mpya za kushughulikia misitu kupitia tangazo la serikali namba 417 (GN 417).

Tulisema ukizisoma kanuni hizo katikati ya mstarini kama zinaondoa mamlaka ya halmashauri za vijiji kuamua namna ya kusimamia misitu iliyo katika vijiji vyao na madaraka hayo kuyapeleka kwenye mamlaka za kiserikali, hususani kwa Mkurugenzi wa Misitu.

Tulishaangalia pia namna bei elekezi ya mkaa inayotokana na kanuni hizo mpya ilivyoanza kukimbiza wafanyabiashara katika vijiji vinavyovuna mkaa kwa njia endelevu, wakielekea kwenye maeneo ambayo kuna uvunaji holela au kwenye vijiji vilivyo karibu na soko lao.

Halikadhalika, tulisikia wadau wanavyosema kuhusu hatua hiyo ya serikali kuhusu faida na hasara wanazoziona. Leo tunaendelea na mtazamo zaidi wa viongozi na wadau mbalimbali walipoulizwa swali hili: Ni upi mtazamo wako kutokana na hatua ya serikali kuondoa mamlaka ya vijiji kuamua namna ya kushughulikia misitu iliyoko kwenye maeneo yao na madaraka hayo kuzipa mamlaka za serikali kuu. 

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mvomero ambako kuna vijiji vitano vinavyoendesha Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM), Mwalimu Mohammed Utaly anasema: Hatua hiyo inaweza kuwa na pande mbili kwa mtazamo wangu. Upande mzuri na mbaya ingawa pengine wanaopendekeza hilo wanaweza kuwa na maelezo mazuri zaidi.

Uzuri wa hilo anasema ni kwa baadhi ya vijiji ambavyo havina mipango mizuri ya usimamizi shirikishi wa misitu na havina utaalamu, lakini havitaki kuomba utaalamu huo. Kwa vijiji kama hivyo, Mwalimu Utaly anasema huenda hatua hiyo ikawa na manufaa.

Lakini hatari ya hatua hii ni kuwaondolea wanavijiji sense of ownership(hisia za kumiliki msitu yao). Inapotokea wanakijiji wakaona kama msitu sasa si mali yao tena, hapo kuna hatari zake katika ulinzi wa misitu,anasema.

Mwalimu Utaly anashauri kwa vijiji vinavyofanya usimamizi shirikishi ni vyema vikaachiwa kusimamia na kufanya maamuzi ya misitu yao wao wenyewe na hilo kuwa sharti kwa kijiji kinachotaka kujiamulia namna ya kuendesha misitu yao. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro anayemaliza muda wake, Kibena Kingo, anapinga hatua hiyo ya serikali kuondoa mamlaka ya vijiji kusimamia misitu na kuishauri kuwa na utaratibu wa kupeleka elimu ya uvunaji endelevu wa misitu kupitia dhana ya usimamizi shirikishi katika vijiji.

Nasema hivyo kwa sababu mpaka sasa serikali haijawa na utaratibu mbadala ambao utawafanya watu wote wasitumie misitu kwa njia isiyo endelevu. Rasilimali misitu kwa ajili ya mbao, magogo, kuni, mkaa na fito ni vitu ambavyo tunaendelea kuvitumia kwa mahitaji yetu na hivyo ni lazima misitu itaendelea kuvunwa.

Lakini misitu inapovunwa kwa njia endelevu inakuwa ni vizuri sana, lakini unapoanzisha utaratibu wa kuwanyanganya wanavijiji mamlaka ya kusimamia misitu yao kwa njia endelevu, unaweza kuwafanya warudi kwenye kuvuna holela,anasema.

Mwenyekiti huyo wa halmashauri ambaye pia alikuwa diwani wa Kata ya Ngerengere anasema kwa sasa halmashauri yao ina vijiji vitano vinavyoendesha usimamizi shirikishi wa misitu kupitia Mradi wa Kuleta Mageuzi Katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) maarufu kama mkaa endelevu, rafiki wa mazingira.

Baada ya kuona manufaa makubwa ya mpango huu, kwenye bajeti yetu ya halmashauri ya mwaka 2019/20 tumepanga kuanza na kijiji kimoja zaidi cha Sesenga ili viwe sita.

Misitu hii inazungukwa na watu. Hawa ni watu ambao wamezaliwa katika maeneo hayo vizazi na vizazi na wamekuwa wakifanya shughuli zao, ikiwemo kuvuna misitu japo kuna maeneo ambayo misitu hiyo imekuwa haisimamiwi vizuri.

Ikumbukwe serikali kuu haina uwezo wa kusimamia misitu yote nchi nzima na hivyo ni vyema misitu ikaendelea kusimamiwa kwa uhuru kabisa na vijiji isipokuwa tupeleke katika kila kijiji mikakati kama hii ya uvunaji wa misitu kwa njia endelevu na ulinzi wake,anasema.

Anasema wananchi ukiwaelimisha, kisha ukawaandalia mazingira kama ilivyofanyika kwenye vijiji vya mradi, watajua kwamba hii ni raslimali yao inayowanufaisha na hivyo hakutakuwa na matumizi mabaya ya misitu.

Lakini leo ukisema misitu hii sasa irudi kwenye usimamizi wa serikali kuu moja kwa moja utawafanya wafanye uvunaji holela mkubwa na hata hujuma kwa sababu serikali haitakuwa na uwezo wa kulinda misitu kwani hata ile ambayo iko chini yao wanashindwa kuisimamia ipasavyo kutokana na nguvu kazi ndogo walio nayo.

Mimi ninafikiri serikali ingejipanga kuja kujifunza kwenye vijiji vya miradi na kueneza hii elimu Tanzania nzima ya kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi na hatimaye kuanzisha usimamizi shirikishi wa misitu huku vijiji vikibaki na uhuru wa kuamua mambo yao kwani nimeona huu mpango una mafanikio makubwa sana, siyo tu kwa vijiji vya halmashauri yangu bali hata katika maeneo mengine kama Kilosa na Mvomero,anasema. 

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai anasema usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji ndio unaofaa kwa sasa kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kusimamia vijiji vyote nchi nzima.

 

Wilaya ya Kilwa pekee ina ukubwa takribani kilometa za mraba13,000. Yaani wilaya hii inakaribia kulingana na Mkoa wa Mtwara wenye eneo la kilometa za mraba 16,000. Kwa hiyo utaona tuna eneo kubwa sana ikiwemo misitu. Kwa hali kama hiyo usitarajie kwa rasilimali tulizo nazo kama wilaya kuweza kufanya doria za mara kwa mara ili kukabiliana na uharibifu katika eneo lote la misitu.

Anaendelea:Tunashukuru kazi inayofanywa na Wakala wa Misitu (TFS) katika kulinda misitu ambayo iko chini ya serikali, tunashukuru pia taasisi zisizo za kiserikali kama MCDI ambao wametusaidia katika kutoa elimu kwa wanavijiji kufanya usimamizi shirikishi wa misitu. Lakini kama nilivyosema tuna eneo kubwa ambalo hata ukifanya doria hakuna barabara za kupita kwa magari lakini serikali hizi za kijiji zikikaa imara ndizo tunazozitegemea kufanya ulinzi wa misitu.

Anasema misitu ya vijiji kusimamiwa na serikali kuu kunaweza kuwa na faida ya mapato kuja serikali kuu na kumrudia tena mwakijiji na hata kuvifikia vijiji ambavyo havina misitu.

Lakini hili halionekani kwa macho kwa mwananchi wa kawaida kule kijijini Nanjirinji, Likawage au pale NakiuDhana itakayokuwepo ni kunyanganywa misitu yao. Wataona msitu siyo wao tena bali wa serikali, ni wa umma, ni wa wote. 

Ikumbukwe wao ndio walikuwa wanaulinda, wanavuna kwa njia endelevu wanashirikishwa kwa njia zote. Leo unasema msitu huu unasimamiwa na mamlaka fulani ya serikali, hii itapunguza molari wa wananchi katika utunzaji wa misitu yao.

Baya litakalojitokeza pale baada ya wananchi kujivua wakiona sasa msitu wao, kuna hatari ya misitu yetu hii kuangamia kwa kasi ya ajabu sana. Sasa wanaweza kuwa watu wazuri kushirikiana na wavunaji haramu katika kuvuna misitu. 

Hata raia wema waliokuwa wakitunza ule msitu watageuka na kuamua kuivuna holela kwa dhana ile ya kila mtu achukue chake mapema. Kwa hiyo gharama ya kutunza hii misitu itakuwa ni kubwa sana.

Mimi kwa maoni yangu, ningeona tuwajengee uwezo zaidi hawa watu wa vijiji kama tunataka msitu ilindwe kupitia sense of ownership, kuwapatia rasilimali na kuwashirikisha zaidi katika utunzaji wa misitu hii,anasema.

Itaendelea

MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya England 2020/2021 umeanza na ...

foto
Mwandishi: Hamisi Kibari

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi