loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Namungo yamkataa Tangalu

BAADA ya Namungo FC kumsajili Fred Tangaru kwa mkataba wa miaka miwili, kocha wa timu hiyo, Hitimana Thierry amesema usajili huo siyo mapendekezo yake.

Namungo wamemsajili nyota  huyo kutoka Lipuli FC kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika ikiwa ni mwanzo wa kuimarisha kikosi kujipanga na msimu ujao wa Ligi Kuu na kuiwakilisha nchi kimataifa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Thierry alisema usajili uliofanywa hajashirikishwa na wala hawajazingatia ripoti yake aliyowapa baada ya msimu kumalizika.

“Baada ya kumalizika msimu, nilitoa ripoti ambayo nilibainisha upungufu na mahitaji yanayotakiwa ili  kuimarisha kikosi kwa msimu ujao na  kimataifa lakini nimeshangaa kuona wamemsainisha mchezaji ambaye hayupo kwenye mapendekezo yangu,” alisema.

“Mimi bado nipo Dar es Salaam, sijaondoka kurudi kwetu Rwanda lakini hawajanipigia simu kuniuliza au kuhitaji maoni yangu nashangaa,“ alisema Thierry.

Thierry alisema mapendekezo aliyotoa kwa uongozi ni wachezaji wazoefu kwenye idara zote akitolea mfano kiungo Lukas Kikoti anahitaji kupata msaidizi, safu ya ulinzi pamoja na safu ya ushambuliaji.

“Mapendekezo ni muhimu ndani ya kikosi changu hakuna mchezaji mzoefu na tunakwenda kwenye michuano mikubwa ambayo inashirikisha timu zenye wachezaji wengi wenye ubunifu na kutumia maarifa uwanjani,” alisema Thierry.

Alisema hata mazungumzo yanayoendelea kati ya Jaffari Mohamed aliyetemwa na Yanga hajashirikishwa ingawa alisifia ubora wake na kudai hakuwepo kwenye mapendekezo yake.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi